KATIBU Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change Taifa (ADC) Doyo Hassani Doyo akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni
KATIBU Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change Taifa (ADC) Doyo Hassani Doyo kulia akiwa kwenye picha pamoja na viongozi wa vyama vyengine vya siasa katikati ni Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Christina Mndeme hivi karibuni
…………………………………………………………………………….
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change Taifa (ADC) Doyo Hassani Doyo amesema Rais Samia Suluhu ni kiongozi shupavu,mvumilivu kwa sababu Urais sio nafasi ndogo huku akiendeleza tunu ya umoja na amani ikiwemo kuiwezesha nchi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.
Doyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Mahusiano ya Baraza la vyama vya Siasa Tanzania aliyasema hayo wakati wa mahojiano ambapo alisema utendaji wa Rais Samia Suluhu ni mzuri kutokana na kasi kubwa ya maendeleo inayoendelea hapa nchini inaonekena na matunda yake yamekuwa na faida kwa watanzania.
Alisema kwa sababu malengo na maono yake ni maono ya mashauriano na ya kuwaweka pamoja huru wananchi kitendo ambacho kitachochea kasi ya maendeleo hapa nchini ikiwemo kufungua milango kwa wawekezaji ambao wanataka kuwekeza hapa nchini.
“Kama kiongozi wa kisiasa ninampongeza Rais Samia kwa hatua ambazo amechukua tokea kuwa Rais katika kipindi hiki kubwa kwa kuwa mvumilivu na shupavu kwa sababu kuwa Urais sio nafasi ndogo na hatujawahi kuwa na Rais mwanamke kwenye Taifa letu”Alisema
Alisema kwa sababu hiyo ni mara ya kwanza kitengo cha miezi sita nchi kutulia na inapiga hatua kubwa kiuchumi na kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake kwa upande wake ni hatua kubwa na anampongeza sana Rais Samia Suluhu.
Katibu huyo alisema kwa mtazamo wake Rais Samia ni chanya wenye faida na malengo na maono yake ni ya mashaurino na kuwaweka watu pamoja na kuwaweka watu awe huru na Tanzania salama ambao unatija kubwa kwa watanzania.
“Lakini pia mtazamo wangu Rais Samia Suluhu kama Rais mwelekeo wa kisiasa unaleta matumaini makubwa sana nchini na sioni kama kuna tatizo kwani hata nchi ambazo zimeendelea kama Marekani,Denmark na Sweeden baada ya uchaguzi chama kilichopewa dhamana na wananchi kinafanya shughuli za maendeleo na siasa inakuja wakati wa uchaguzi”Alisema Katibu huyo.
Aidha alisema hata Rais wa awamu ya tano Marehemu Dkt John Magufuli alimtumia majukwaa kuhimiza maendeleeo na kujenga heshima kwenye nchi na hivyo kwa mtazamo wangu naona hakuna tatizo kwenye upande wa siasa hapa nchini.