Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Vijana, Kazi na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akifafanua jambo katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama mahala pa kazi katika UKumbi wa Bunge, Jijini Dodoma, Oktoba 21, 2021.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia mada mbalimbali zil;izokuwa zikiwasilishwa katika kikao cha kamati hiyo na Wataalam kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika UKumbi wa Bunge, Jijini Dodoma, Oktoba 21, 2021.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa sheria ya afya na usalama mahali pa kazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Jijini Dodoma, Oktoba 21, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Kazi na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu akieleza jambo katika kikao hicho. Katikati ni Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Kazi na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka (Mb.) (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge akieleza jambo wakati wa kikao hicho walipokutana kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama mahala pa kazi katika UKumbi wa Bunge, Jijini Dodoma, Oktoba 21, 2021.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)