Mgeni rasmi wa mahafari ya 7 ya Kilimani sekondari mwaka huu, Meneja wa NHIF Kanda ya ZIwa, Jarlath Mushashu,akizungumza na wazazi,walimu, wahitimu watarajiwa na wanafunzi (hawapo pichani)
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani, Gerana Majaliwa, akisoma risala ya shule hiyo kwa mgeni rasmi Jarlath Mushashu (mwenye koti), kushoto,wakati wa mahafari ya 7 ya wahitaimu wartarajiwa wa shul hiyo
Mwanafunzi Slyvester George akiwa na mama yake mzazi wakati akipokea cheti cha mshindi wa jumla baada ya kuibika kinawa wa Masomo ya Kemia, Baiolojia, Fizikia na Hesabu kati ya wahitimu watarajiwa wa Kilimani Sekondari
Mwalimu wa Taaluma na mwalimu wa somo la Kemia,Atanas Manyika, kipokea cheti cha mwalimu aliyefaulisha vizuri kwenye masomo. Picha na Baltazar Mashaka
………………………………………………………
NA BALTAZAR MASHAKA, Ilemela
SHULE ya Sekondari Kilimani,katika Manispaa ya Ilemela, inahitaji sh.milioni 40 kutatua changamoto za upungufu wa miundombinu ya madarasa,hosteli,matundu ya vyoo,vitendea kazi na samani za ofisi.
Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Shule hiyo, Gerana Majaliwa, kwenye risala ya shule hiyo kwa mgeni rasmi wa mahafari ya 7 ya wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne, mwaka huu.
Alisema shule hiyo ina upungufu wa vyumba 6 vya madarasa,matundu 30 ya vyoo,meza na viti 216 vya wanafunzi,viti na meza 12 za walimu,vatanda kwa ajili ya hosteli, kopmyuta 3,mashine ya kudurufu maandishi,ujenzi wa hosteli ya wasichana yenye uwezo kuchukua wanafunzi 120 kwa wakati mmoja,wanafunzi kukosa bima ya afya na.
Majaliwa aliitaja changamoto nyingine ni maji ya bomba kutoka kwa kusuasua na kusababisha kuvurugika kwa ratiba za masomo,hivyo kuwalazimu wanafunzi kufuata huduma hiyo umbali mrefu nje ya shule na uendelezaji wa miundombinu mipya ya shule kunakokwamishwa na eneo kutopimwa.
Mkuu huyo wa shule alisema Bodi ya Shule imepitisha mikakati ya miaka mitano ili kuzitatua changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu iliyopo na kuiwekea sakafu na vigae,hivyo nguvu za pamoja kati ya jamii,wazazi,uongozi wa shule na wadau mbalimbali zinahitajika.
“Utatuzi wa changamoto hizo unahitaji sh. milioni 40 zitakazotumika kuboresha na kujenga miundombinu ya madarasa,vyoo,kununua samani za shule na vitendea kazi vitakavyowawezesha walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza katika mazingira bora,hivyo kukuza taaluma na kuongeza ufaulu,”alisema Majaliwa.
Alieleza pamoja na changamoto,Kilimani Sekondari imekuwa na mafanikio mazuri ya kitaaluma ambapo mwaka 2020 matokeo ya mitihani ya kitaifa, kidato cha nne, ufaulu uliongezeka hadi asilimia 97.9 kutoka asilimia 94.7 mwaka 2019.
Pia idadi ya waliojiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya kati pia iliongezeka kutoka 42 mwaka 2091 hadi 88 mwaka 2020 huku wanafunzi 25 wakifaulu daraja la kwanza huku mwaka 2019 kidato cha pili ufaulu ukiongezeka kutoka asilimia 93.8 hadi kufikia asilimia 96.5, mwaka 2020.
Kwa upande wake mgeni rasmi, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Ziwa,Jarlath Mushashu,kabla ya kuendesha harambee ya kukusanya sh. milioni 40, alisema suala la malezi ya watoto wazazi wamewaachia walimu na kuwataka wazazi kutumia karama waliyobaki nayo kuwalea watoto ambao ni jamii na taifa la kesho,wawe waadilifu,wakiwaachia watakuwa wanajenga taifa lenye matatizo.
Alisema watoto wengi wamepotea kwa kutolelewa vizuri na kwamba suala la maadili kwenye jamii halisistizwi,mzazi akiwa hana maadili tusitarajie mtoto atakuwa na maadili,hivyo wanawajibika kushirikiana na walimu kuwalea watoto na karibu nao,wawaonyeshe njia watimize ndoto zao za maisha kwani shule ya kwanza huanzia nyumbani.
Aliwaasa wahitimu hao watarajiwa kuwa watakuwa nyota jinsi walivyojiandaa kwenye masomo ili wafikie malengo waliyojiwekea na ajira yoyote inahitaji nidhamu,uvumilivu na uadilifu,japo vikwazo ni vingi visiwakatishe tamaa, wavivumilie kwani kila kitu kinachokuja kinatokana na bidii.
Mushashu ambaye alivutiwa na mafanikio ya kitaaluma ya shule ya Kilimani na mpango wa kujenga hosteli,alisema jamii,wananchi,wazazi na wadau wanawajibu wa kuunga mkono maendeleo ya shule hiyo na kuwataka kufanya kitu cha kukumbukwa kwa wahitimu wa shule hiyo mwaka huu, kwa kuchangia fedha na vifaa ili kuboresha miundombinu na kununua vifaa ili kukuza taaluma na kuongeza ufaulu.
“Nimeona Kilimani kuna uongozi thabiti wenye maono na mipango ya maendeleo ya kitaaluma,mmejipanga kuiweka shule ya Kilimani kwenye kiwango cha juu miaka mitatu ijayo kutokana na ushirikiano wa jamii, walimu na wanafunzi,tutawaunga mkono ili kuacha alama hapa na suala la wahitimu kufaulu liko mikononi mwao kwa namna walivyoajiandaa,”alisema.
Meneja huyo wa NHIF aliwaongoza wageni mbalimbali,wazazi, walimu, wanasiasa wakiwemo wabunge na madiwani kuchangia ambapo alichangia sh.40,000 kwa kula keki, Mbunge wa Ilemela, Dk. Angeline Mabula(sh.100,000).