Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa wamachinga Taifa Bw.Steven Lusinde akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho leo Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa wamachinga Taifa Bw.Steven Lusinde akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho leo Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Shirikisho wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Yusuph Namoto akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho leo Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limeiomba Serikali kuwashirikisha viongozi wa Umoja huo kwa kuwa wanawajibu wa kuishauri Serikali katika kufanya maboresho ya changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali wanamofanyia biashara ili kuhakikisha wamachinga wanakuwa na mazingira bora ya biashara.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa wamachinga Taifa, Steven Lusinde wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vurugu za wamachinga zilizotokea jana katika soko la Kariakoo.
“Viongozi Serikali wanatakiwa wawashirikishe machinga maeneo wanayotakiwa kwenda kuwaweka ili kuondoa sintofahamu pamoja na kuweka muunganiko mzuri na viongozi wa Kundi hili na si kutoa ushirikiano wa Zimamoto”.Amesema
Sanjari na hilo Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma) limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane nao kumweleze kero walizonazo huku wakimuelezea Rais Samia kuwa ndiye Rais wa kwanza kutenga fungu la fedha kwa ajili ya maendeleo ya wamachinga na ambapo ametenga Sh5 bilioni kwa ajili ya manufaa ya wajariamali wadogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Namoto amesema wameona kuna haja ya kutolea ufafanunuzi kwa sasa kwa kuwa ni wa kakati muafaka ili kutolea ufafanuzi kwa yale yaliyoamriwa na Serikali katika eneo la ushauri kama kuna uhitaji.
Wakielezea kuhusu tukio la jana la Kushambuliwa kwao wakati wakishiriki zoezi la kutoa elimu kwa wafanyabiashara wenzao viongozi hao wa wamachinga wamesema wamefanikiwa kwa asilimia 90% ila wale walioonyesha utovu wa nidhamu si wamachinga bali ni kikundi fulani cha wahuni.