Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) Bw. Francis Mapugilo akizungumzia maandalizi ya Shindano la kumpata Mr. Tanzania 2021 linalotarajia kufanyika Oktober 22 Mwaka huu jijini Dar es Salaam.
*************************
Shindano la kumtafuta Mr.Tanzania limeendelea kupamba moto baaada ya waandaji kueleza kuwa maandalizi yote yamekamilika, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kushiriki katika shindano hilo linalotarajia kufanyika siku ya Ijumaa October 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi ya Shindano hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF), Bw. Francis Mapugilo, amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Bw. Mapugilo amesema kuwa washiriki wote wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza saa 7:00 asubuhi kwa ajili ya shindano la kumtafuta Mr.Tanzania 2021.
Amefafanua kuwa washiriki wote wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 65 na wale watakaoshindwa kufuata sheria za shindano hilo wataondolewa na kuzuiliwa kwa kuonekana kwenye mashindano ya sasa na yale yajayo.
Katika shindano hilo mshindi wa kwanza atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.5m, mshindi wa pili atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.3m, huku mshindi wa tat atachaguliwa kutokana na aina zote tatu za uzani wa Tsh.1m.
Utaratibu wa migandisho hautakuwa zaidi ya sekunde 60 kwenye onesho la fainali, hivyo ni moja ya vitu vya muhimu ambayo washiriki wanatakiwa kuvifaamu.
“Washiriki wanatakiwa kuzingatia na kuzielewa kanuni za mchezo huo ili waweze kuchaguliwa kwani miongoni mwa vigezo vitakavyotumika ni kujua taratibu na kanuni za mchezo huu” amesema Bw. Mapugilo.
Mchezo wa kutunisha misuli ni kama michezo mingine ambayo inaongeza ajira kwa vijana, hivyo vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kushiriki.