Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS Prof Andrea Pembe akikabidhi tuzo ya shukurani kutoka kwa mtoto wa marehemu Ahmed Salim Meneja Masoko wa Mfuko wa Amne Salim mara baada ya mfuko huo kuchangia kiasi cha Shilling Milion 100 kwa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa ajili ya kusaidia tafiti zinazoendelea za ugonjwa wa Uviko 19 hafla ya makabidhiano imefanyika leo Jumatano Oktoba 20,2021 chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS Prof Andrea Pembe akizungumza katika gafla hiyo iliyofanyika katika chuo cha MUHAS jijini Dar es salaam leo Jumatano Oktoba 20,2021.
Picha ya pamoja
………………………………….
Katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kupambana na magonjwa mbalimbali, Mfuko wa Amne Salim umechangia kiasi cha Shilling Milion 100 kwa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa ajili ya kusaidia tafiti zinazoendelea za ugonjwa wa Uviko 19.
Mfuko wa Amne Salim umechangia kiasi hicho ili kusaidia katika tafiti zinazofanywa na Watafiti kutoka MUHAS kupitia ugonjwa wa Uviko 19.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS Prof Andrea Pembe amesema Wanafurahi kuungana na mfuko wa Amne Salim ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani Dkt Salim Ahmed Salim utakaowawezesha wataalam kufanya tafiti kuhusu ugonjwa Uviko 19.
Prof Pembea amesema, Hatua hiyo ilyofanywa na Mfuko wa Amne Salim utahamasisha watu weng wenye nia njema kuunga mkono tafiti za Uviko 19 zinazofanywa na Chuo cha MUHAS.
“Hii itasaidia watafiti wachanga na wanaoibuka kufanya tafiti zao ambazo zinakuja kuleta majibu chanya kwa jamii na kutambua namna ya kupambana na magonjwq,”amesema
“Tafiti hizi zitasaidia ushindani na uwajibikaji ndani ya Taasisi katika kuelewa,kujilinda, kupambana na athari za ugonjwa wa Uviko 19,”
Prof Pembe amesema, ugonjwa wa Uviko 19 umetikisa sekta ya afya, rasilimali na maendeleo ya nchi yameelemewa na kuwa tafiti hizi zitawasaidia kugundua ukubwa wa tatizo, viashiria na athari za ugonjwa huu kwa jamii.
Kwa upande wa Familia ya Marehemu Amne Salim, Mtoto wake Ahmed Salim amesema mfuko huo umeunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na Uviko 19 kwa kuchangia kwenye tafiti zinazofanywa na Chuo cha MUHAS.
Salim amesema, mfuko huo utatoa kiasi cha Milion 100 kwa muda wa miezi 12 kuanzia Oktoba 2021 ili kusaidia tafiti za Uviko 19 na kutambua athari zinazosababishwa na ugonjwa huo.
Familia ya Dkt Salim Ahmed Salim imeamua kufanya kumbukumbu ya kifo cha Mpendwa wao Amne Salim aliyefariki Oktoba 20, 2020
Chuo cha MUHAS kimeweza kumkabidhi mtoto wa Amne Salim Tuzo ya ushirikiano wao na kutambua mchango kwa ajili ya mapambano ya Uviko 19 kupitia tafiti watakazozifanya.