Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,akiwahimiza viongozi wa Mkoa wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Maganga,akielezea lengo Kuu la Mkutano wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Best Magoma ,akizungumzia hali ya utoaji wa Chanjo wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Mratibu wa Chanjo mkoa wa Dodoma Francis Bujiku,akitoa taarifa ya mwenendo wa UVIKO-19 kwa waliopata chanjo na wasiopata chanjo kulingana na Tafiti wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Afisa Afya wa Mkoa wa Dodoma Nelson Rumbeli,akielezea mikakati ya kuongeza kasi ya uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri ,akichagia mada wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya,akichagia mada wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dodoma Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu,akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19 kilichofanyika leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amezitaka kamati za afya za wilaya zote kuweka mikakati ya kufikisha elimu ya chanjo katika maeno yote juu ya umuhimu wa uchanjaji wa Uviko -19.
Hayo ameyasema leo Oktoba 18,2021 jijini Dodoma wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi cha Mkoa kufanya Tathmini juu ya mpango jamii shirikishi na harakishi wa Chanjo ya Uviko-19.
”Hakikisheni kuwa huduma hizo zinawafikia wananchi katika maeneo yote yenye mikusanyiko kama sehemu za Ibada Misikitini,Makanisani, kwenye Makongamano sambamba na sehemu za vituo vya Mabasi”amesema Mtaka
Mtaka amesema kuwa ofisi ya Mkoa tayari wameshapokea shehena mpya ya chanjo ya Sinopharm dozi elf 50,390.
“Sasa hizi kamati ziende huko sehemu ambapo watu wapo mkatoe elimu juu ya chanjo hii mpya baada ya ile nyingine kuisha mkawape elimu na wataalamu pia mkatoe elimu juu ya chanjo hii” amesema Mtaka.
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo mkoa wa Dodoma Francis Bujiku amesema Mkoa wa Dodoma awali ulipokea jumla ya dozi 50,000 za chanjo ya Uviko 19 ya JJ na mnamo tarehe 3 Agosti 2021 ulizindua kampeni ya uchanjaji na hadi kufikia tarehe 5 oktoba Mkoa ulikua umemaliza chanjo zote zilizopangwa kwa asilimia 100.
“Baada ya kuona tumemaliza zile zilizopangwa tukaomba chanjo za ziada 6515 kutoka Mikoa ya Geita chanjo 5000,Iringa1515 na mpaka kufikia Oktoba 13 jumla ya wananchi 52,599 walichanja chanjo ya Uviko 19” amesema Bujiku
Amesema kufuatia uanzishwaji wa chanjo ya Uviko 19 katika Mkoa wa Dodoma tarehe 3 Agosti 2021wananchi wamepata elimu na vituo viliongezeka 28 vya kutoa chanjo na badae kuongezeka hadi kufikia 381, ambapo walengwa 52,629 wamepatiwa chanjo hadi kufikia tarehe 14 oktoba 2021sawa na asilimia 93 ya lengo la kuchanja walengwa 56,515.
Kuhusu uanzishwaji wa chanjo mpya Bujiku amesema Serikali imejipanga kuwa na utaratibu wa utekelezaji wa uanzishwaji wa chanjo hiyo mpya ya Sinopharm ambao utaleta matokeo makubwa.
Hata hivyo Bujiku amesema kuwa vituo 381 vitaendelea kutumika kutoa chanjo hiyo pamoja na huduma ya mkoba katika maeneo yote ambapo chanjo hiyo itatolewa Mara 2 dozi hiyo ya pili itatolewa siku 28 baada ya chanjo ya kwanza huku akiwasisitiza wananchi kutopuuzia kurudi kumalizia dozi hiyo ya pili.