Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Watalii ( TATO) , Willy Chamburo mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha Shilingi milioni 150 kwa Waziri huyo ikiwa ni pesa ambayo ni makusanyo yaliyofanywa na TATO kwenye vituo vya kutolea sampuli kwa ajili ya vipimo vya corona kwa wageni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kipindi cha mwaka jana, hafla hiyo ya kukabidhi hundi imefanyika jana Jijini Arusha huku ikishuhudiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer ( wa kwanza kulia)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia) akizungumza na Wadau wa utalii pamoja na Wataalam mbalimbali walioshiriki katila mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini ambapo ameahidu kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kushoto) akiwa na
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer ( kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (European Business Group)
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer akizungumza na Wadau wa utalii pamoja na Wataalam mbalimbali walioshiriki katila mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (European Business Group), Cikay Richards akizungumza na Washiriki wa mkutano wa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini kabla ya mkutano huo kuanza
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia ) Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer ( katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu wa masuala ya utangazaji utalii pamoja na Wadau wa Utalii nchini mara baada ya kumaliza mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini
………………………………………………………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Watoa huduma za Watalii kuwa mstari wa mbele kuchanja ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya UVIKO 19
Pia,Dkt.Ndumbaro amesema kitendo cha Watoa huduma wengi katika sekta ya utalii kuchanja ni jambo la muhimu kwani watalii wanaokuja nchini wanapata ujasiri kuwa nchi wanayotembelea ni salama na hivyo hawawezi kupata maambukizi
Ametoa wito huo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya ( European Business Group) uliowakutanisha Wadau mbalimbali wa Utalii nchini kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili sekta ya utalii nchini
Katika mkutano uliwaokutanisha wataalamu mbalimbali kwa upande wa Serikali uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro huku kwa upande Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ulaya uliongozwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer
Dkt.Ndumbaro amefafanua kuwa watalii waingiapo nchini huhitaji huduma kama vile malazi, chakula uongozwaji, starehe kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii pamoja na kununua bidhaa mbalimbali za kiutamaduni kwa ajili ya matumizi yao na kubeba kama zawadi, ni muhimu watu wa sehemu hizi kuchanja ili kujilinda
Ameongoza kuwa Watu wote wanaotoa huduma katika maeneo hayo wanawajibika kuwa mstari wa mbele kuchanja ili kuendelea na shughuli za utalii bila kuhatarisha afya na maisha yao na wanaowapa huduma .
” Wanatoa huduma ambao hawajachanjwa wapo hatarini zaidi kupoteza maisha yao kwa vile wanakutana na watu wa kutoka mataifa mbalimbali duniani hususani yale ambayo yana maambukizi makubwa ya UVIKO 19, Nawasihi kwa usalama wa maisha yao wachanje” amesisitiza Dkt.Ndumbaro
” Lazima mtambue kuwa watalii wengi hutokea nchi za Ulaya, Amerika na Asia ambazo hadi wakati huu bado zina viwango vya juu vya maambukizi ya UVIKO 19” alisisitiza Dkt. Ndumbaro
Amesema tangu Serikali ya Tanzania iliporidhia kupokea chanjo watalii wameanza kumiminika kuja nchini kwa vile wanaujasiri kwa kuamini kuwa sehemu wanayokwenda ni salama kwa ajili ya afya zao, tunamshukuru sana
Hata hivyo , Dkt.Ndumbaro amewataka watoa huduma kwa watalii wale waliochanja na wale ambao bado kuendelea kuzingatia taratibu zilizowekwa na Wizara hiyo pindi wanapowahudumia watalii kuhakikisha wqnachukua tahadhari zote ikiwemo kuvaswanavaa barakoa muda wote.
Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema Wizara anayoiongoza imeshaanza mazungumzo na Wizara ya Afya, Jinsia na Watoto kuona uwezekano wa kuwaruhusu watalii wanaokuja nchini ambao wamepimwa ndani ya masas 72 na waliochanjwa kutokupima tena pindi wanapowasili katika viwanja vya ndege na mipakani.
Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wieber de Boer amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa namba moja katika kutoa ajira nchini ikiwemo kutoa mafunzo pamoja na kujenga miundombinu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu sekta ya utalii kama ilivyosaidia kujenga Chuo cha Taifa cha Utalii pamoja na kuandaa miongozo ya kutangaza sekta ya utalii inayotumika nchini
” Uholanzi ni Wadau wakubwa wa maendeleo katika nchi hii hususani katika masuala ya utalii tunaiahidi Serikali kuendelea kushirikiana kwa namna yoyote ile hasa katika nyakati ambazo sekta ya utalii imeshambuliwa na UVIKO 19” alisisitiza Mhe. Balozi Boer