Dada Mkuu wa shule ya Wasichana Kondoa ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha sita Mariamu Kassim akisoma risala ya shule hiyo kwa Mgeni rasmi Afisa Mkuu wa Fedha kutoka TANESCO Renata Ndege .
Afisa Mkuu wa Fedha kutoka TANESCO Renata Ndege akipokea risala kutoka kwa Dada Mkuu wa shule ya Wasichana Kondoa ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha sita Mariamu Kassim.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa baada ya kutoa msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 shuleni hapo.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akiwahimiza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa kusoma kwa bidhii pamoja na kupenda masomo ya Sayansi wakati wa hafla ya kukabidhi misaada mbalimbali katika shule hiyo leo Oktoba 16,2021.
Makamu Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa,Alvin Lema,akiishukuru TANESCO kupitia Tuico wanawake Makao Makuu kwa kuwakabidhi Misaada mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi.
Kaimu Mwenyekiti wa TUICO Tawi la Makao Makuu Idara ya Wanawake Neema Mbuja,akielezea jinsi walivyoguswa mpaka wakaleta misaada mbalimbali katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wakifatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kukabidhiwa Misaada mbalimbali kutoka TANESCO kupitia Tuico Wanawake Makao Makuu leo Oktoba 16,2021 wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akikabidhi Komputa kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa,Alvin Lema pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo wakipokea ambapo TANESCO kupitia Tuico Wanawake wametoa msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 shuleni hapo.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akikabidhi Kitanda pamoja na ambapo TANESCO kupitia Tuico Wanawake wametoa msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,pamoja na Tuico Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Kondoa mara baada ya kukabidhi msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 shuleni hapo.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akipanda Mti katika Shule ya Wasichana Kondoa,mara baada ya kutoa msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 shuleni hapo.
Dada Mkuu wa shule ya Wasichana Kondoa ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha sita Mariamu Kassim,akiipongeza TANESCO kupitia Tuico Wanawake kwa kupokea msaada wa Komputa na Vitanda.
Makamu wa Rais wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kondoa ,Diana Mfanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka kutoka TANESCO kupitia Tuico Wanawake.
Waziri Mkuu Msaidizi katika shule ya Wasichana ya Kondoa,Theresa Adolf,akitoa wito kwa Taasisi pamoja mashirika mengine kuiga mfano wa TANESCO katika kusaidia shule mbalimbali zenye mahitaji.
Afisa Mkuu wa Fedha TANESCO Renata Ndege,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda Mti katika Shule ya Wasichana Kondoa ambapo TANESCO kupitia Tuico Wanawake wametoa msaada wa Komputa,Vitanda,Magodoro pamoja na mashuka hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 16,2021 shuleni hapo.
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Kondoa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia Tuico wanawake Makao Makuu wametoa msaada wa Komputa,vitanda vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 pamoja na kuwafunda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa kupenda masomo ya Sayansi
Akizungumza leo Oktoba 16,2021 wakati wa makabidhiano hayo Afisa Mkuu wa Fedha kutoka TANESCO Renata Ndege amesema hiyo ni mara ya pili kupeleka msaada katika shule hiyo ambapo wamekabidhi Komputa na vitanda vya Dispensary vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23.
“Tumekuja Kondoa Girls kikubwa tumekuja kuwasalimia kuongea nao mabinti zetu, tumekuja kama wanawake wa Makao Makuu wa Tawi la TUICO tumekuja kwa niaba ya shirika zima kuwaletea misaada.
“Kikubwa tumeleta Komputa pamoja na vitanda vya Dispensary vyenye thamani yazaidi ya shilingi milioni 23 hii ni mara ya pili mara baada ya kutupa changamoto zao kwani tulikuja mwezi wa tatu walitueleza changamoto zao tofauti tofauti,”amesema.
Amesema Shirika linatamani kuwa na mafundi wengi wanawake hivyo wamefika shuleni hapo kuwahamasisha kusoma kwa bidii ikiwemo masomo ya Sayansi.
“Kina mama inawezekana, wajitahidi kwenye mchepuo wa sayansi kwani ukiangalia Shirika letu tunatumia mafundi wengi . Tunatamani tuwe na Wahandisi wengi katika shirika letu tumefurahi sana na wanachangamoto zao kama Shirika tutaendelea kutoa misaada,”amesema Bi.Renatha
Hata hivyo ametoa wito kwa Mashirika na Taasisi zingine kuiga mfano wa Tanesco kuzisaidia shule zenye mahitaji ili kuwasaidia wanafunzi kuweza kufikia ndoto zao.
“Wito wetu kwa mashirika ama taasisi zingine ambao wana uwezo ni kwenda katika mashule kama haya kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufikia malengo yao tukisaidiana tutawafikisha mbali katika kuhakikisha tunakuza elimu,”amesema.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Shule ya Wasichana Kondoa,Alvin Lema amesema wanashukuru kwa msaada huo kwani awali walipokea misaada mbalimbali ikiwemo taulo za kike kutoka katika Shirika hilo.
“Tumepokea msaada kutoka Tanesco awali tulipokea misaada mbalimbali lakini leo tumekabidhiwa vitanda 10,magodoro 8 ,mashuka na Komputa 10 huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwa sababu tuna Dispensary hivyo vitanda vilikuwa vinahitajika.
“Pia,tunashukuru kwa Komputa kwani tunaenda kwa sasa katika teknolojia vifaa hivi tutavitumia vizuri na tunaahidi hatutawaangusha na vifaa hivi vitatusaidia kuboresha matokeo yetu katika mitihani ya kitaifa tunajua hivi vifaa vitawasaidia sana kwani wataingia katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.
“Taasisi zingine niwatake hii shule ni ya kwao unapokuja na kutusaidia umeisaidia Tanzania kwani wasichana hawa watafanya kazi katika taasisi ambazo zipo na milango ipo wazi,”amesema.
Naye,Kaimu Mwenyekiti wa TUICO Tawi la Makao Makuu Idara ya Wanawake Neema Mbuja amesema wameleta msaada shuleni hapo kutokana na shule kufanya vizuri katika mitihani yake hivyo wanajukumu la kuwasaidia watoto hao wa kike kutimiza ndoto zao.
“Kikubwa tulivutiwa kuja kutoa huu msaada kwa sababu tuliona ni watoto wenye mahitaji hivyo tuliona ni bora kuja kushirikiana nao katika kile kidogo.
“Tumeleta msaada kwa sababu kwanza shule inafanya vizuri lakini sisi kama TUICO tunalojukumu la kuwasaidia wanawake kwa ajili ya kuhakikisha wanasimama wapende masomo ya sayansi sisi ni mama zao ni dada zao tumekuja kuwatia moyo kwamba elimu ndio msingi wa kila kitu,”amesema.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Msaidizi katika shule ya Wasichana ya Kondoa,Theresa Adolf ameishukuru TANESCO kwa kutoa misaada katika shule hivyo wameahidi kusoma kwa bidii ili ndoto zao ziweze kutimia.
Amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa gari la wagonjwa hivyo wanaziomba Taasisi zingine ikiwemo na Tanesco waweze kuwasaidia.
Naye,Makamu wa Rais katika shule hiyo,Diana Mfanga amesema wanashukuru kwa msaada huo lakini wanaomba wasaidiwe waweze kupata internet ili waweze kupata huduma mbalimbali.
“Kama wakiweza isiwe hapa kwetu tu waende na shule zingine ili waguse maisha ya kila mwanamke hasa sisi ambao ni mabinti sisi ndio Taifa la Tanzania la kesho,”amesema
Kwa upande wake Dada Mkuu wa shule hiyo ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha sita Mariamu Kassim amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Shirika la Tanesco linafika hapo lilipo ambapo ametoa rai kwa mashirika mengine kuwasaidia wanafunzi hasa wenye mahitaji maalum.
“Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Tanesco kwa msaada huu wa Computa tunaahidi tutazitumia vizuri nitoe rai kwa Mashirika mengine kuwasaidia watu wenye uhitaji naamini kuna shule mbalimbali ambazo zinauhitaji,”amesema.