Na Lucas Raphael,Tabora
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega mkoani Tabora imewahukumu watu 5 kutumikia kifungo cha miaka 30 kwa kila mmoja baada ya kupatikana na kosa la kujeruhi na unya’nganyi wa kutumia siraha
Akitoa hukumu hiyo jana na hakimu mkazi wa wilaya ya Nzega Mhere Mwita hakimu huyo alisema kutokana na ushahidi usioacha shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia adhabu hiyo.
Hakimu huyo alisema kutokana na kukidhiri kwa matendo ya uharifu mahakama hiyo inatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao ambapo kila mmoja hatatumikia kifungo hicho cha miaka 30 jela.
Awali wakili wa serikali Jenifa Mandago aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ni namba 113 ya mwaka 2020 ambapo october 27 ya mwezi wa tisa mwaka 2020 majira ya usiku .
Aliwataja watu hao watano kuwa ni Kulwa Kaseme,Josephu Salumu,Mabula Mmoja,Kiswalo Kulwa na Ngasa Mhumbi ambao walivamia kwa Saimoni Bundala mkazi wa kijiji cha Iyombo wilaya ya nzega mkoani hapa wakiwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na kumpiga na kumjeruhi na kisha kumwibia kiasi cha fedha shilingi laki moja.
wakili huyo wa serikali alisema kutokana na ushahidi kukamilika mahakamani hapo anaomba kutolewa adhabu kali kwa watu wao ili iwe fundisho kwao na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo hakimu Mwere Mwita alitoa nafasi ya kujitetea kwa watu hao watano baada ya ushahidi kukamilika ambapo waliomba kupunguziwa adhabu kutokana na kuwa na familia zinazowakabili.
Hata hivyo mahakama hiyo haikuridhia na utetezi huo na imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela kwa kila mmoja baada ya kupatikana na kosa hatia..