RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania Suleiman M.Mzee akitowa maelezo ya Miradi mbalimbali inaotekelezwa na Jeshi la Magereza Tanzania wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Miradi Mnne ya Jeshi hilo katika Gereza la Kingolwira Morogoro leo 15-10-2021 na ( kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martin Shegella na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene wakiondoa kipazia kuufungua Mradi wa Jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika Gereza la Kingolwira Mkoani Morogoro leo 15-10-2021 na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Waziri) Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania Suleiman M.Mzee.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma Jiwe la Msingi la Jengo la Mradi wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto baada ya uzinduzi huo na (kushoto) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuzindua Mradi wa Jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika Gereza la Kingolwira Morogoro leo 15-10-2021 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene na Mkewe Mama Mariam Mwinyi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa Gereza la Mtengo wa Simba Kingolwira Morogoro SP.Awazi D.Mwazembe, akitowa maelezo wa Jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto baada ya kulizindua leo 15-10-2021, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Jengo la Mradi wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Martin Shegella
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa Gereza la Mtego wa Simba Kingolwira Morogoro SP.Awazi D.Mwazembe, akitowa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaazi kabla ya Uzinduzi huo uliofanyika leo 15-10-2021 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe George Simbachawene.(Picha na Ikulu)