Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) Bw. Francis Mapugilo akizungumzia maandalizi ya Shindano la kumpata Mr. Tanzania 2021 linalotarajia kufanyika Oktober 22 Mwaka huu jijini Dar es Salaam.
****************************
Kamati ya Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) imetaja orodha ya mavazi yanayoitajika kwa washiriki watakao shindana kwenye shindano la kumpata Mr.Tanzania linalotarajia kufanyika 2021 October 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kuelekea maandalizi ya Shindano hilo, Katibu Mkuu wa TBBF Francis Mapugilo, amesema kuwa kila mshiriki anatakiwa kuwa na vazi aina ya suti, suruali ya jeans rangi ya bluu au nyeusi pamoja na vazi la migandisho.
“Utaratibu wa migandisho hautakuwa zaidi ya sekunde 60 kwenye onesho la fainali, hivyo ni moja ya vitu vya muhimu kuvifaamu washiriki,”amesema Mapugilo.
Ameeleza kuwa washiriki wa Shindano la Mr.Tanzania 2021 wameatakiwa kujifunza mikakati ya shindano lenyewe kama vile anuwai zilizotajwa kutoka kwenye picha na video zilizochapishwa kwenye akaunti ya Instagram, Facebook na YouTube.
Amesema kuwa washiriki wote wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 65 na watakaoshindwa kufuata sheria shindano wataondolewa na kuzuiliwa kwa kuonekana kwenye mashindano ya sasa na yale yajayo.
“Mshindi wa 1 atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.5m , mshindi wa pili atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.3m, huku mshindi wa tat atachaguliwa kutokana na aina zote tatu za uzani wa Tsh.1m” amesema Mapugilo.
Shindano la MR. Tanzania linatarajia kufanyika October 22 mwaka huu, huku washiriki wote watatakiwa kuripoti katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam siku hiyo kuanzia saa 7:00 asubuhi.