Home Mchanganyiko TAKUKURU DODOMA:’TUTAENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA WALA RUSHWA’

TAKUKURU DODOMA:’TUTAENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA WALA RUSHWA’

0

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,akizungumza wakati akifungua Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mlezi wa klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Maria De Mathias mwalimu Isack Petro,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Afisa Elimu kata Julius Msafiri,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Wanafunzi wakitoa burudani  wakati wa ufunguzi wa Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,akipanda Mti mara baada ya kufungua Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda mti pamoja na kufungua Club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………..

Na. Alex Sonna,DODOMA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere imesema kuwa itaendeleza Mapambano dhidi ya wala rushwa kwa kutumia Sheri kali ambazo zitakuwa mwarobaini kukomesha Vitendo hivyo nchini.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 14,2021 jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,wakati akifungua club ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika Shule ya Sekondari ya Maria Dematias.

Bw.Kibwengo amesema kupitia maboresho ya sheria ambazo zimewekwa baina ya kupokea Rushw ni kosa la uhujumu uchumi ambapo itasaidia kupunguza vitendo hivyo nchini.

“Niwaambie sheria imeboreshwa makosa yote ya rushwa sasa hivi ni makosa ya uhujumu uchumi isipokuwa kosa moja tu la hongo kati ya makosa 24 ni makosa ya uhujumu uchumi” amesema Kibwengo.

Aidha kibwengo amesema kuwa  endapo mtu atabainika amepokea rushwa atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 20 Jela bila Mbadala wa Faini .

“kwa hiyo adhabu sio ndogo kifungo cha miaka ishirini sio kidogo lakini wale waliotenda makosa haya zamani serikali itatumia sheria ile ya zamani kutoa  hukumu  maana makosa yao walitenda kabla ya maboresho haya.

Kwa upande wake  Afisa Elimu kata Julius Msafiri  ameiomba TAKUKURU isiishie shuleni  tu na badala yake iendeleze utamaduni wa kuanzisha club hizo kwenye shule nyingine mkoni Dodoma ili iwe fursa kwa vijana wengine kupata mafunzo ya kupambana na vitendo vya rushwa

“Club hizi zitasaidia kutuondolea tatizo hili la rushwa ambalo lipo tangu tupate uhuru, nikuombe Kamanda wa TAKUKURU uendeleze  warsha kama hizi kwa watoto wa shule za Msingi na Sekondari maana itasaidia kutoa elimu kwao namna ya kupambana na vitendo vya rushwa.”

Idadi ya wanachama 367 kwenye Club ya Marie De Mathias na zimeshiriki Club za Shule 8 na  katika Shule zote za Mkoa wa Dodoma zimeanzishwa Club lengo likiwa  ni kutoa elimu kwa wanafunzi namna ya kupambana na vitendo vya Rushwa  ambao watoto hao ni Taifa la kesho.