Home Mchanganyiko BUTIKU:’TUTAENDELEA KUENZI UONGOZI ULIOACHWA NA HAYATI MWL NYERERE KWA KUONDOA TOFAUTI ZA...

BUTIKU:’TUTAENDELEA KUENZI UONGOZI ULIOACHWA NA HAYATI MWL NYERERE KWA KUONDOA TOFAUTI ZA KIKABILA’

0

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Aliyekuwa Mbunge Mhe.Steven Wasira,akichagia mada wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya “Sisi Tanzania” ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo Medoti Mashaka Medoti,akielezea lengo la  Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa kundi la vijana Mkoa wa Singida Nusrat Hanje,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku amesema miaka 22 bila uwepo wa muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, watanzania wataendelea kuuenzi uongozi wake usiolea sumu kwenye uongozi na kuondoa tofauti za kikabila zilizokuwa zikiitafuna nchi kwa wakati ule.

Hayo ameyasema leo Oktoba 14,2021 Jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake kilichotokea miaka 22 iliyopita nchini Uingereza katika Hospitali ya St.Thomas mwaka 1999.

Butiku ,amemtaja mwl Nyerere kama shujaa wa ujamaa na kujitegemea hivyo kuwataka watanzania kujitegemea na kuacha uvivu utakaokwamisha maendeleo ya familia zao .

Aidha ameeleza kuwa maisha yake yalikuwa ni tunu kwa watanzania kwa kuwa aliishi kwa kusimamia uzalendo,umoja,mshikamano na kujitoa hata kwa kuhatarisha maisha yake.

Hata hivyo  Butiku amesema vijana wa kitanzania wanapaswa kusimama katika nguzo hizo kwa kuzingatia malezi Bora ya wazazi wao na hatimaye kuwa na Taifa linalozingatia utu na maadili .

“Malezi yanawandaa watanzania wenye maadili na utii na kuwa na nafasi ya kukubali kusahihisha au kusahihishwa pale ambapo ni lazima,”amesema Butiku.

Aidha amefafanua  kuwa katika kipindi chote alichafanya kazi na Mwl.Nyerere alimshuhudia akiwajali wanawake kwa vitendo na kuwapa usawa hali iliyowaondolea dhana ya kudharauliwa .

Kwa kufanya hivyo amesema Nyerere aliamua kuandika kitabu cha wanawake ili kuhamasiaha jamii kutambua mchango wa wanawake katika harakati za maendeleo ya taifa.

“Tumeshuhudia Mwalimu akiwapa nafasi za uongozi baadhi ya wanawake akiwepo Titi Mohamed “amesema

Kwa upande wake Mhe.Steven Wasira ameweka wazi kufurahishwa na jinsi vijana wanavyomuenzi Mwl Nyerere kwa kujifunza mambo mengi aliyoyafanya katika kipindi cha  uhai wake.

“Nimefurahi kuona kuwa kuna watu wanaomjua vizuri Mwalimu kama waliishi naye na hii inaonyesha wazi kwamba watanzania wanapenda Viongozi shupavu wanaojali uwajibikaji na uwazi Kama alivyofanya Baba wa Taifa,”amesema Mhe.Wasira

Mbali na hilo ameeleza kuwa Mwalimu Nyerere aliwajali vijana kwa vitendo kwa kumpa kazi kwa nafasi ya ukuu wa Mkoa akiwa na miaka 27 tu.

“Vijana wasioelewa vizuri maono ya mwalimu wanaweza wakababaishwa  kutokana na Dunia ya sasa ya mitandao,maisha mnayoishi sasa mnahitaji kukuwa zaidi kwa kuzingatia ukweli na hapo mtakuwa mmemuenzi ,”ameeleza.

Aidha amesema kutokana na mapenzi na nchi yake Mwalimu alianza harakati za utetezi akiwa bado mwanafunzi Ili kuondoa udini na ukabila ulioanzishwa na Wakoloni .

“Mwalimu alichukia ubaguzi wa kidini ulioanzishwa na wakoloni,wakoloni waliuchukia uislamu kitu ambacho Mwalimu aliopingana nacho na kuanzisha harakati za kupigania uhuru na hatimaye kuwa Taifa huru lisilo na udini,”amesema.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira, ametumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kumuenzi Mwl.Nyerere kwa kuzingatia kilimo chenye tija kwa uhakika wa chakula na lishe.

“Mwalimu Nyerere alipenda sana kilimo,aliamini kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu,hii ilijidhihirisha wakati akitoa mada maalumu huko Roma-Italia ambapo alisisitiza kuwa asilimia 97 ya watanzania kwa wakati ule wengi walitegemea sekta ya kilimo,”anasema.

Mbunge wa kundi la vijana Mkoa wa Singida Nusrat Hanje amesema katika kumuenzi Hayati Mwl.Nyerere lazima kuwaenzi pia Waandishi wa vitabu kwa sababu wamewezesha kizazi cha sasa kumjua vizuri.

“Wengi hatumjui Nyerere lakini kupitia Vitabu tunaweza kumuelezea sifa zake na kumuelewa,kupitia Waandishi wetu mahiri tuaishi kupitia maisha yake”amesema

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya “Sisi Tanzania” ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo Medoti Mashaka Medoti ameeleza lengo la kuandaa jukwaa hilo  ni kuwapa fursa watanzania na hasa vijana kumuenzi Baba wa Taifa, kutafakari maisha yake na kuishirikisha jamii kuona ni kwa namna gani maisha yake yanakuwa chachu katika uchumi wa nchi.

“Tumelipa kongamano hili jina la Vijana na mwalimu Nyerere,tunatumia jukwaa hili kutoa mustakabali wetu kama vijana kwa kuziishi fikra zake hasa kwa kuzingatia katika harakati zake alitumia nusu ya maisha yake kuhudumia watanzania kwa kujitoa na kufanya misingi ya ujenzi wa Taifa letu kuwa na dhana ya kuheshimu utu wa binadamu,”amesisitiza

Hata hivyo Bw.Medoti  amesema kwa miaka 22 bila uwepo wa Hayati Baba wa Taifa hilO, watanzania wana kila sasababu za kujivunia kama taifa lenye mshikamano uliorithishwa.

“Katika hili tuna deni la kulipa kwa kushikamana kushirikiana katika kukemea ujinga na maradhi,tunamuenzi na kumkumbuka zaidi kwa uongozi wake usiolea sumu kwenye taifa letu na kuondoa tofauti za kikabila zilizokuwa zikiitafuna nchi kwa wakati huo,”amesema .