Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kibaha Tulitweni Mwinuka wa kulia aliyeshika mkasi akikata utepe kwa ajili ya sherehe za makabidhiano rasmi kutoka kwa Taasisi ya Al- SwadiQ Al- amen Foundation ambayo imefadhili ujenzi wa zahanati hiyo kwa wananchi wa mtaa wa Miwaleni Kaata ya Visiga kushoto kwake ni kiongozi wa taasisi hiyo Shekh Said Chega.
Afisa mtendaji wa kata ya Visiga Alloisia Nyello wa kushoto akiwa ameshika zawadi maalumu ya cheti kwa ajili ya kumkabidhi kiongozi wa taasisi hiyo kwa kuweza kutoa sapoti kubwa katika kufanikisha mradi wa ujenzi huo wa zahanati.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Kibaha mji Tulitweni Mwinuka akizungumza jambo katika halfa hiyo ya kukabidhiwa rasmi mradi wa zahanati kwa wananchi wa mtaa wa miwaleni.
Kiongozi wa Taasisi hiyo Shekh Said Chega kulia akitia saini makubaliano baina ya tasisi hiyo pamoja na halmashauri ya mji wa kibaha ikiwa ni makabidhiano rasmi.
Diwani wa Kata ya Visiga Mbugu Legeza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na ujenzi wa zahanati hiyo.
Kulia ni mwanasheria Riziki Majala akiwa anatoa mwongozo wa kusaini kwa kiongozi huyo wa taasisi pamoja na mganga mkuu wa halmashauri ya mji kibaha.
…………………………………………………..
VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANANCHI wa mtaa wa miwaleni uliopo Kata ya Visiga katika Halmashauri ya mji wa Kibaha mkoani Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa kipindi cha zaidi ya miaka 55 hatimaye wanatarajia kuondokana na kutembea umbari wa kilometa 15 kwa ajili kufuata huduma ya matibabu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa zahanati mpya.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Visiga Mbegu Legeza kwa niaba ya wananchi wake wakati wa halfa ya makabidhiano ya jengo la zahanati hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Kiiislam ya Al- SwadiQ Al-Ameen Foundation kwa ajili ya kuikabidhi rasmi kwa uongozi wa serikali ya halmashauri ya mji Kibaha ili iweze kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wa kata ya Visiga na maeneo mengine ya jirani .
Diwani huyo alibainisha zahanati hiyo ambayo imejengwa katika mtaa wa miwaleni itasaidia kuwapunguzia kero na adha kubwa ambayo walikuwa wanaipata wananchi katika kipindi cha miaka ya nyuma kutokana na kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya matibabu katika maeneo ya mbali.
Aliongeza kuwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia kuboresha sekta ya afya hasa kwa wananchi ambao wananchi katika maeneo ya pembezoni na kwamba mradi huo utaweza kuzinufaisha kaya zaidi ya 400 katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu.
“Mimi kama Diwani wa kata hii pamoja na Afisa mtendaji wangu wa kata pamoja na wananchi kwa ujumla tumefarijika sana kwa ujio wa zahanati hii maana ni zaidi ya miaka 50 sasa wananchi hawa katika mtaaa huu walikuwa hawana huduma ya zahanati kwa hiyo hii taasisi imeweza kufanya jambo la muhimu sana katika kuisaidia jamii ambayo inatuzunguka na sisi tunaendelea kushirikiana nao,”alisema Diwani huyu.
Kwa upande wake kiongozi wa taasisi hiyo Shekh Said Chega amesema kwamab wameamua kujenga mradi wa zahanati katika eneo hilo kutokana na kuguswa na kubaini kuwepo kwa changamoto za huduma ya upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa mtaa huo kwa kutumia muda mwingi kwenda kutibiwa katika maeneo ya mbali.
Pia kiongozi huyo alifafanua kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wanashirikiana naa serikjali katika kuanzisha miradi mbali mbali ya kimaendeleo lengo ikiwa ni kuwasaidia wananchi ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika Nyanja mbali mbali na kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
“Taasisi yetu inashughulika na mambo mbali mbali hasa katika kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta ya afya, elimu, maji na mambo mengine yanayohitajika kwa hivyo sisi tulibaini uwepo kwa wananchi wa mtaa huu kusumbuka katika huduma ya afya na ndio maana tukaamua kujenha zahanati hii ambayo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 70,”alisma kiongozi huyo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kibaha akipokea jengo hilo la zahanati kwa niaba ya serikali amebainisha kuwa mradi huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na kuwataka kuhakikisha wanailinda miundombinu yote na kuachana kabisa na vitendo vya kufanya hujuma na wizi wa vifaa mbali mbali katika zahanati hiyo kwani imejengwa kwa ajili yao.
Afis mtendaji wa kata ya Visiga Aloisia Nyello akusita kutoa pongezi zake za dhati kwa uongozi mzima wa Taasii hiyo na kubainisha kwamba mradi huo wa zahanati ni moja ya hatua kubwa katika kuwasogezea huduma wananchi ya matibabu na kwamba mpaka kukamili kwake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 70 na utaweza kuwasaidia wwakazi wa maendeo mbali mbali.
KUKAMILIKA kwa mradi huo wa ujenzi wa zahanati ya mtaa wa Miwaleni iliyopo kata ya Visiga Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kutaweza kuwaondolea changamoto ya wananchi kutembea umbari wa kilometa 15 pamoja na kuzisaidia kaya zaidi ya 400 kupata huduma ya matibabu kwa uhakika zaidi