Home Mchanganyiko ONESHO LA VYAKULA VYA AFYA NA LISHE LAFANYIKA KIJIJI CHA USARE MKOANI...

ONESHO LA VYAKULA VYA AFYA NA LISHE LAFANYIKA KIJIJI CHA USARE MKOANI KILIMANJARO

0

Gradianus Mgimba Mganga Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro akizungumza na wananchi katika kijiji cha Usare kata ya Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambako kumefanyika Siku ya Afya na Lishe  kwa kufanya onesho maalum la vyakula vya Asili na Virutubisho ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani iliyozinduliwa na na Mkuu wa mkoa wa Kiliamnjaro Ndugu Steven Kagaigai Oktoba 12, 2021 na itafikia kilele chake Oktoba 17 katika viwanja vya Madela Pasua mjini Moshi.

Dkt. Nyamizi Bundala Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na wananchi katika kijiji cha Usare kata ya Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambako kumefanyika Siku ya Afya na Lishe  kwa kufanya onesho maalum la vyakula vya Asili na Virutubisho.

Jacqueline Machangu kutoka mfuko wa umoja wa. Mataifa wa uendelezaji kilimo (IFAD) akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye  maadhimisho hayo ya Afya na Lishe katika kijiji cha Usare. 

Gradianus Mgimba Mganga Mkuu Mkoa wa Kilimanjaro akipata maelezokutoka kwa wajasiriamali mbalimbali  na wananchi waliofanya onesho maalum la vyakula vya Asili na Virutubisho ikiwa ni Siku ya Afya na Lishe katika kijiji cha Usare kata ya Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Bi. Stella Kimambo Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) tawi la Tanzania akimuonesha maharage ya Lishe Anna Swai mkazi wa kijiji cha Usare aliyehudhuria katika onesho hilo la Afya na Lishe.

Maofisa mbalimbali wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa uendelezaji kilimo IFAD wakigawa uji Lishe kwa watoto waliohudhuria katika onesho hilo la Afya na Lishe katika kijiji cha Usare wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya vkaula Lishe vilivyooneshwa katika kijiji cha Usare wilayani Hai.

Bi. Stella Kimambo Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) tawi la Tanzania akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kijiji cha Usare mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wafanyakazi wa FAO na IFAD waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

Wananchi wa kijiji cha Usare wakimpokea mgeni rasmi ambaye ni Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Gradianus Mgimba wakati alipowasili kijijini hapo.

Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Gradianus Mgimba wakati alipowasili kijijini hapo kuhudhuria maadhimisho hayo ya Afya na Lishe.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Chakula Duniani FAO, IFAD na Wizara ya Kilimo wakiwa tayari kwa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe katika kijiji cha Usare.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Usare waliohudhuria katika maadhimisho hayo.