MBunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka Akizungumza na wananchi wa kata ya Kongowe ikiwa ni ziara take ya kikazi ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi.
…………………………………..
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha katika kuunga juhudi za serikali katika kuleta Chachu ya maendeleo amechangia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3 kwa lengo la kuweza kuchochea Kasi ya maendeleo katika sekta mbali mbali.
Koka ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkutano wa adhara kwa wananchi wa kata ya Kongowe ambayo pia ilikuwa na lengo la kusikiliza kero Cha changamoto zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge huyo ambaye pia ameongozana na viongozi mbali mbali wa halmashauri ya mji wa Kibaha pamoja na wakuu wa taasisi ili kuweza kuzijibu changamoto ambazo zinajitokeza katika Mambo ya maji.elimu.afya na huduma za kijamii.
Aidha katika ziara hiyo Koka aliweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo na kuikagua ikiwemo kujionea miradi ya shule ya msingi miembe saba pamoja na ujenzi wa kituo Cha afya Ungindoni.
“Nipo katika ziara yangu katika kata hii ya Kongowe lakini katika miradi yote ya maendeleo ambayo nimeipitia nitachangia kiasi Cha shilingi laki tano na hii ni kuchochea Kasi ya maendeleo kwa wananchi,”alisema Koka.
Aidha Koka alibainisha kuwa kwa Sasa atahakikisha anapambana vilivyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wake kuweza kupata huduma ya maji Safi na salama.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo aliwaahidi wananchi hao kuboresha miundombinu yote ya barabara ili iweze kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi Cha mvua hasa katika sehemu za njia zinapoelekea zahanati.vituo Cha afya na hospitali.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kongowe Hamisi Shomari amemshukuru Mbunge huyo kwa kuweza kutembelea Chachu ya maendeleo kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria katika mkutano huyo wamempongeza Mbunge huyo kwa juhudi zake na kumwomba awasaidie zaidi katika changamoto ya maji,migogoro ya ardhi sambamba na nishati ya umeme.