Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akifafanua jambo kwa Makatibu Wakuu wa Wizara mbili, Prof. Sifuni Mchome (Katiba na Sheria) na Dkt. John Jingu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) pamoja na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kigoma, Mhe. Athumani Matuma Kirati wakati wa Ziara yao ya kuona jinsi Mahakama inavyofanya kazi, kujua changamoto na kutafuta ufumbuzi. Kikao hicho kilifanyika Mkoa wa Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Thobias Andengenye akieleza Jambo mbele ya Makatibu Wakuu wa Wizara tatu, Prof. Sifuni Mchome (Katiba na Sheria), Dkt. John Jingu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) na Christopher Kadio (Mambo ya Ndani ya Nchi) waliomtembelea wakati wa Ziara yao mkoani Kigoma.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kigoma, Mhe. Athumani Matuma Kirati akitoa maelezo ya Utendaji wa Mahakama Kanda ya Kigoma mbele ya Makatibu Wakuu wa Wizara tatu, Prof. Sifuni Mchome (Katiba na Sheria), Dkt. John Jingu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) na Christopher Kadio (Mambo ya Ndani ya Nchi) waliofanya ziara Mahakamani hapo kuona utendaji kazi wa Mhimili huo wa Dola wa Kanda ya Kigoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akizungumza jambo katika Kikao kazi cha Mpango wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), Manispaa ya KigomaUjiji. Kikao hicho kilichoshirikisha Katibu Mkuu wa Afya (Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio kimefanyika tarehe 13 Oktoba 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akimkabidhi fedha Katibu wa Wazee Wasiojiweza katika Makazi ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji mara baada ya Ziara yao ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara, Profesa Sifuni Mchome na Christopher Kadio waliofika kwenye Makazi hayo kubainisha changamoto zinazowakabili ili kutafuta ufumbuzi wa pamoja.