Kamishna Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Amina Talib akizungumza na wanafunzi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto yaliyofanyika UKumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mratibu wa jinsia tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora Ofisi ya Makao makuu Dodoma akiwasilisha mada ya udhalilisha wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wanafunzi juu ya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto huko Ukumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya ukatili naudhalilishaji kwa wanawake na watoto yaliyoandaliwa na tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora huko Ukumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka Skuli ya John Pombe Magufuli akichangia mada kuhusu ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto katika mafunzo ya kuwajengea uelewa yaliyofanyika katika UKumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Warda seif Othman akichangia mada kuhusu ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto katika mafunzo Ya kuwajengea uelewa yaliyofanyika Ukumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka skuli ya Legezamwendo Ali Mohammed akichangia mada kuhusu ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto katika mafunzo ya kuwajengea uelewa yaliyofanyika katika UKumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Afisa elimu Wilaya ya MAghribi “A” Fatma Sleyyum Abeid akichangia mada kuhusu ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto katika mafunzo ya kuwajengea uelewa wanafunzi yaliyofanyiaka Ukumbi wa maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR
……………………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo
Kamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Amina Thalib Ali amesema ukatili na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto humuathiri mtendewa wa vitendo hivyo kiakili kimakuzi na kimalezi pamoja na kupelekea kuipoteza haki yake ya elimu ipasavyo.
Alisema vitendo hivyo ambavyo vinaendelea kushamiri hapa Zanzibar huathiri vijana ambao ndio tegemeo la taifa la kesho .
Aliyasema hayo katika mafunzo ya haki za binaadamu na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe, ambayo yaliwashirikisha wanafunzi mbali mbali kutoka skuli za msingi na sekondari zilizopo wilaya ya magharibi A na B.
Aidha alisema jumla ya kesi 868 zilizoripotiwa kwa mwaka huu na 567 ni za watoto wa kike sawa na asilimia 68 jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya taifa.
Kamishna huyo aliwataka wanafunzi hao kueleza matatizo mbali mbali wanayokumbana nayo katika jamii ili kutafutiwa ufumbuzi muafaka kupitia tume hiyo kwa lengo la kuzishauri serikali zote mbili kutokana na changamoto hizo zinazojitokeza.
Kwa upande wa wanafunzi hao walisema uelewa mdogo wa wazazi na walezi katika jamii kuhusu vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia unapelekea vitendo hivyo kuzidi kuengezeka.
Walisema kutokana na umasikini na hali duni ya maisha ,mporomoko wa maadili kwa kuziacha mila desturi na tamaduni za awali pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii huchangia kuwa na tamaa kwa wanafunzi na hupelekea kufuata ushawishi na ulaghai ambao huchangia vitendo hivyo.
Nao Wanafunzi hao walitoa wito kwa wazazi na walenzi kuwa karibu na watoto wao kwa kuwapa ushauri na mbinu za kuepukana na vitendo hivyo vinavyowapotezea ndoto zao .