Home Biashara WAKULIMA WILAYANI MANYONI WATAKIWA KUUZA KOROSHO ILIYOBANGULIWA

WAKULIMA WILAYANI MANYONI WATAKIWA KUUZA KOROSHO ILIYOBANGULIWA

0

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Mh. Hussein Bashe akizungumza na wakulima wa Korosho akiwa katika ziara wilayani Manyoni mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Mh. Hussein Bashe akizungumzkikagua mashamba ya wakulima wa Korosho wilayani Manyoni mkoani Singida.

Wakulima Wilayani Manyoni wametakiwa kuondokana mtazamo wa kuuza Korosho ghafi na badala yake sasa kuanza kuuza korosho iliyobanguliwa.

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Mh. Hussein Bashe ameeleza hayo Mapema leo wakati alipokuwa akifanya kikao katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa.

Akizungumza na viongozi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melekzedeki Humbe, pamoja na wataalamu wa kilimo Manyoni

Bashe amesema kuwa anawapongeza kwa utekelezaji wa malengo ambayo Wilaya ya Manyoni imefanya kwani waliweza kujiwekea lengo la kulima hekari elfu 32 na mpaka sasa hekari elf 22 zimekwishapandwa.

Bashe amesema kuwa Manyoni na Central koridol yote Wizara imeelekeza kuwa ni sehemu ya ubanguaji hivyo Wizara ya Kilimo na Halamashauri na Wilaya wameweka makubliano kuwa Halamashauri ya Manyoni na Wilaya itajenga Ghala na Wizara italeta vifaa kwa ajili ya ubanguaji.

Aliongeza kuwa Wizara itaasaidia katika kuuza korosho zilizobanguliwa badala ya kuuza korosho ghafi na amesema kuwa lengo ni kumsaidia mkulima wa manyoni kuweza kupata thamani ya zao lake.

“Tunataka tuwasidie katika ubanguaji ili mkulima wa korosho aweze kupata thamani halisi ya zao lake”alisema BasheAidha kuhusu changamoto zinazowakabili wakulima hao

 Bashe amesema kuwa changamoto ya wakulima ni viwatilifu hivyo ameaagiza kutengeneza Amcos ya wakulima wa korosho ili Serikali iweze kuona namna ya kuwasaidia kupata ruzuku kidogo ili iweze kuwasaidia gharama za kulea zao.

“Tumekubaliana watengeze umoja wao na ushirika wao amcos halafu tutaangalia ni namna gani tunawaingiza katika pakage za kuwapa ruzuku kidogo kama Serikali ili kuwapunguzia gharama za kulea zao kwa sababu wanatakiwa walilee kwa miaka mitatu kwa hiyo ile (Capital Intensive) ni kubwa mno wanayowekeza kama wakulima kwani wanasafisha mashamba kama mnavyoona ,wanaajili vibarua na sasa wanahitaji msaada Serikalini, kwa hiyo sisi kama Wizara tutakuwa hatujawatendea haki wakulima wa aina hii ambao wameonyesha moyo na Halmashauri ya aina hii ambayo imeonyesha tija namna hii kushindwa kuwasaidia katika kuendeleza mradi wao”alisema Bashe

Aidha ameongeza kuwa makubaliano mengine waliyoweka ni pamoja na kuchimba visima katika mashamba yao ili kuweza kupata maji ya kuchanganyia viwatilifu kwa karibu zaidi.Kuhusu viwatilifu amesema kuwa Wizara imewapatia lita 410 za Duduba leo ili ziweze kusaidia katika kupunguza wadudu wanaoshambulia mazao hayo.“lakini kazi inayofanyika Manyoni inatakiwa kuungwa mkono na sisi kama Wizara tutaendelea kuwaunga mkono, Comintmenti yetu ni korosho ya Central koridal iuzwe katika ubanguaji na wala siyo kuuza korosho ghafi na hili linawezekana”alihitimisha Bashe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa amesema kuwa anashukuru sana Serikali kwa kuona tija ya kuendelea kuimarisha mradi wa kilimo cha korosho Manyoni.

Pia ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa malengo na mikakati ambayo imeweka ili kuweza kuinua na kudumisha kilimo cha korosho manyoni na hasa suala la uchimbaji wa visima vya maji kwani ndiyo kilio kikubwa kwa akulima wengi. “niseme kwamba tumefurahi sana na tunaishukuru Wizara kwani kwa sasa baada ya visima hivyo kuchimbwa changamoto za maji zitapungua sana na wakulima wataweza kuhudumia mashamba yao kiuhakika” alisema Mwagisa

Naye Francis Alfred Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya korosho Tanzania amesema kuwa watashirikiana na Halmshauri kuhakikisha korosho ya Manyoni inabanguliwa ili kutekeleza mpango wa Serikali.

Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedek Humbe ameishukuru Serikali pamoja na Wizara na amesema kwamba watashirikiana na Serikali ili kuweza Kuimarisha na kukuza mradi huu wa ubanguaji korosho Wilaya ya Manyoni.