Home Mchanganyiko WAHADZABE WAOMBA CHANJO YA UVIKO-19

WAHADZABE WAOMBA CHANJO YA UVIKO-19

0
Joseph Lyimo
WAOKOTA matunda, warina asali, wawindaji wa asili wa jamii ya pembezoni wakihadzabe wanaoishi bonde la Yaeda Chini, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wameiomba Serikali kuwapatia chanjo ya kupambana na jangwa la Uviko-19.
Mkazi wa kijiji cha Mongoamono, John Yamungu amesema jamii ya wahadzabe wanaoishi kwenye bonde la Yaeda Chini nao wanapaswa kupatiwa chanjo ili wajikinge na Uviko-19.
Amesema kuwa jamii hiyo nayo inahaki ya kupatiwa chanjo kama watu wengine wanavyopatiwa hapa nchini japokuwa wenyewe siyo watembeaji kwa kuzunguka maeneo mbalimbali.
Amesema suala la kupambana na janga la Uviko-19 ni jambo la kila mmoja hivyo wahadzabe nao wanapaswa kupatiwa chanjo hiyo ili wasiathirike na ugonjwa huo unaoua.
“Uviko-19 hauchagui mtu, jamii wala kabila, hivyo wahadzabe nao wanatakiwa kupatiwa chanjo hiyo ya Uviko-19 na kujikinga na changamoto hiyo inayotishia dunia kwa sasa,” amesema.
Hata hivyo, mmoja kati ya wakazi hao Singo Jumbayu ameeleza kuwa jamii hiyo inapaswa kupatiwa elimu ya Uviko-19 kwani wahadzabe mara nyingi shughuli za kitaifa huzigomea.
“Huwa wanajali mno utamaduni wao hivyo shughuli ya kuwaelimisha inapaswa  kufanyika kwani wahadzabe wana msimamo mkali nakumbuka kipindi cha sensa kikifika huwa wanataka seikali iwachinjie wanyamapori ndiyo washiriki,” amesema.
Amesema kutokana na shughuli ya chanjo ni yakitaifa na inapaswa kufanyika nchini kote jamii ya wahadzabe wanapaswa kuelimishwa na kupatiwa chanjo ya Uviko-19.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Abukary Kuuli amesema wamepokea dozi 2,000 za chanjo ya Uviko-19.
Kuuli amesema mwitikio wa watu kuchanja ni mkubwa kwani zimeshatumika dozi 1,300 kwa watu mbalimbali kufika mahospitalini, vituo vya afya na zahanati kupatiwa chanjo.
“Changamoto inayotukabili ni baadhi ya madhehebu kudai kuwa bado wanasubiri kibali kutoka kwaviongozi wao ili  washiriki kupata chanjo hiyo ya Uviko-19,” amesema Kuuli.
Amesema kila siku kuna watu watatu hadi wanne wanafika kwenye ofisi yake kuuliza namna ya kupata chanjo hiyo ya Uviko-19 na kuelekezwa eneo  la kupata huduma hiyo.
Amesema jamii ya pembezoni ya wahadzabe wa Yaeda Chini tayari nao wamepewa kipaumbele kwa kufikishiwa chanjo ili wachanje na kujikinga na janga la Uviko-19.
“Hivi ninavyozungumza na wewe tayari chanjo imeshapelekwa na kufikishwa kwa jamii ya wahadzabe ili nao waweze kupatiwa chanjo ya Uviko-19.