Home Mchanganyiko TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YANADI TOZO ZA UMWAGILIAJI

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YANADI TOZO ZA UMWAGILIAJI

0

 
Kushoto
ni Afisa Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi Christina
Mwasaka akifafanua jambo kwenye kipeperushi kwa washiriki wa Ofisi hiyo
katika Banda, ndani ya Maonesho yanayoendelea Mjini Moshi katika viwanja
vya shule ya Msingi Mandela, kuelekekea maadhimisho ya siku ya Chakula
Duniani.
Afisa
Kilimo Mwandamizi kutoka Idara ya Uendeshaji Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji Bw. Mohamed Mcheni, akifafanua Jambo kwa waandishi wa Habari
hawapo katika picha, kwenye maonesho yanayoendelea mjini Moshi kuelekea
kilele cha maadhimisho ya siku ya chakula Duniani.
 
 
Na Mwandishi Wetu – Moshi
 
Ushiriki
wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika maonesho yanayofanyika mjini
Moshi kuelekea maadhimisho ya siku ya chakula Duniani, yameipa fursa
ofisi hiyo kunadi sera zake kwa wananchi zinazowataka kisheria wakulima,
kulipa tozo za kilimo cha umwagiliaji.
 
Akizungumza
na baadhi na wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo, Bw. Mohamed
Mcheni Afisa Kilimo Mwandamizi amesema kuwa, taratibu zote za ukusanyaji
wa ada umekamilika na kutangazwa katika gazeti la serikali, “Kwa mwaka
huu wa fedha na miaka inayoendelea tutaendelea kukusanya asilimia tano
(5%), na kabla ya kulipa, skimu inatakiwa isajiliwe.” Alisisitiza.
 
Aidha,
Bw. Mcheni alisema kuwa Asilimia tano hiyo ni sawa na wastani wa gunia
moja kwa hekari kwa zao la mpunga na aliendelea kufafanua kuwa, chama
cha wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji zinatakiwa kulipa
ada ya usajili kiasi cha shilingi laki moja na elfu sabini na tano
(175,000/-) ambapo shilingi laki moja ni ada ya mwaka na shilingi elfu
sitini ni ada ya usajili, na shilingi elfu kumi na tano ni ada ya maombi
ya usajili.
 
Alitoa wito kwa wakulima kulipa ada ya asilimia tano (5%) ya wastani wa mavuno kwa msimu wa mwaka kwa hekari.
 
Maonesho
kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya Chakula Duniani yenye kauli
mbiu unayosema inayosema “Zingatia Uzalishaji na Mazingira Endelevu kwa
lishe na Maisha Bora” yanafanyika Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro katika
kiwanja cha shule ya msingi Mandela.