Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza leo na Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizoshinda zabuni za kuanza usafishaji wa eneo ujenzi wa Kambi na Kiwanda cha kupakia rangi bomba na ile iliyopewa jukumu la ulinzi katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP)
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo ya utangulizi leo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuzungumza na Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizoshinda zabuni za kuanza usafishaji wa eneo ujenzi wa Kambi na Kiwanda cha kupakia rangi bomba na ile iliyopewa jukumu la ulinzi katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP)
Mhandisi wa Ujenzi wa Bomba Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP) Jose Ayllon akitoa ufafanuzi leo jinsi wanavyotarajia kuanza kazi ya awali za ujenzi wa Bomba hilo mapema mwezi ujao kwa kuanza na usafishaji wa eneo la ujenzi wa Kambi na kitakapojengwa Kiwanda cha kupakia rangi mabomba.
Baadhi ya Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizoshinda zabuni za kuanza usafishaji wa eneo ujenzi wa Kambi na Kiwanda cha kupakia rangi bomba na ile iliyopewa jukumu la ulinzi katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora(hayupo katika picha) walipokutana naye leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kumaliza mazungumzo leo na Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizoshinda zabuni za kuanza usafishaji wa eneo ujenzi wa Kambi na Kiwanda cha kupakia rangi bomba na ile iliyopewa jukumu la ulinzi katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP)
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………………
NA TIGANYA VINCENT,TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka Wakandarasi wote waliopata zabuni ya kuanza ujenzi wa Kambi ya Sojo na Karakana katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki( EACOP) kuweka makazi ya kuishi wilayani Nzega ili wakazi wa eneo waanze kufaidi fursa za ujenzi wa mradi huo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati alipokutana na Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizoshinda zabuni za kuanza usafishaji wa eneo ujenzi wa Kambi na Kiwanda cha kupakia rangi bomba na ile iliyopewa jukumu la ulinzi
Alisema wafanye kazi katika eneo Sojo, wanapokwenda kulala watumie Nyumba za Wageni na Hoteli zilizopo katika Wilaya ya Nzega na sio katika Wilaya nyingine.
Balozi Dkt. Batilda alisema hali hiyo itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha kwa wakazi wa Wilaya ya Nzega watakaotoa huduma mbalimbali na kuwaletea maendeleo.
Aliongeza kuwa na kwa upande wa ajira ikiwemo Wasafishaji wa eneo la ujenzi wa mradi na ujenzi wa Kambi na Karakana ya kupaka rangi bomba na ulinzi kipaumbe wapewe Vijana wanaozunguka mradi kwani watasaidia pia katika suala la ulinzi.
Balozi Dkt. Batilda alisema kama kutakuwepo na mapungufu kwenye huduma wanazihitaji, uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na wa Wilaya ya Nzega upatiwe taarifa mapema kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
“Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kila wakati anasisitiza wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali kuzingatia ‘Local Content’ ili watu wa eneo husika waweze kunufaika na utekelezaji wa mradi …kwetu sisi tunawasisitiza kutumia huduma zote zinazopatikana Nzega na kulala Nzega na sio kwingine ili watu wetu waweze kunufaika fursa ya ujenzi wa bomba hilo” alisisitiza
Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali ya Mkoa wa Tabora imejipanga kutoa ulinzi wakati wote wa utekelezaji wa ujenzi wa mradi na baada ya kumalizika kwake na kuongeza kuwa watakapoona kuwepo viashiria vya kuleta matatizo watoe taarifa ili hatua zichukuliwe.
Kwa upande wa Mhandisi wa Ujenzi wa Bomba hilo Jose Ayllon alisema kazi ya awali zinatarajia kuanza mapema mwezi ujao kwa kuanza usafishaji wa eneo la ujenzi wa Kambi na kitakapojengwa Kiwanda cha kupakia rangi mabomba.