……………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Isdor Mpango amewaagiza wakuu wa mikoa inayomwaga maji mto Rufiji kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika bonde la mto huo, ili kulinda ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika bwawa la Mwalimu Nyerere -Rufiji,uliofikia asilimia 48.
Amewaagiza wakuu hao wa mikoa ikiwemo Pwani na Morogoro, kuchukua hatua kwa wale wote wanaochoma misitu ovyo, shughuli zinazohatarisha mazingira pamoja na mifugo holela.
Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa bwawa la kuzalisha umeme -stigo Rufiji ambalo litazalisha umeme Megawatt 2115 ,Mpango alieleza wakuu wa mikoa hiyo ikiwemo Pwani na Morogoro wadhibiti changamoto hizo ili mradi uweze kuwa na maji ya kutosha .
“Mshughulikie hili bwawa ni zuri tusiriharibu ,Nina taarifa kuna jitihada mnazichukua kudhibiti hali hii ,lakini ongezeni nguvu kuwa mazingira safi “
Bwawa hili lina faida kubwa kwa watanzania ,tunataka umeme wa kutosha nchini ,utalii na umwagiliaji,hivyo tulinde mazingira na kudhibiti uchafuzi wa mazingira,”alifafanua Mpango.
Mpango alibainisha ,ana wasiwasi Kuna uchomaji holela ,wasimamie hili kulinda Kodi ya watanzania ndio wanachangia Kodi na kusababisha miradi hii mikubwa kuleta maendeleo na kuinua uchumi.
“Nimeona leo mlale na agizo hili, kwakuwa umeme ni kila kitu,Mimi ndio msimamizi wa mazingira nisipoona mnalisimamia nitatumia rungu jingine ”
Aidha Mpango amewaelekea mainjinia waongeze wafanyakazi na endapo wakiona changamoto za mradi kuhakikisha wanazitatua kwa wakati.
Pamoja na Hilo,aliwapongeza vijana wa kitanzania waliopata ajira kwenye ujenzi huo ,kwenda sambamba na teknolojia mpya za kujenga ujenzi wa miradi mikubwa na amewataka wawe mfano wa kuigwa.