Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) Mhe. Martin Ngoga akifungua Mkutano wa Kwanza, Kikao cha tano, Bunge la nne ulioanza leo Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) pamoja na wabunge wengine wa Bunge hilo wakifuatilia Mkutano Kwanza wa (Eala), leo Jijini Arusha
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Mhe. Wanjiku Muhya kutoka Kenya akichangia hoja kuhusu Kamati ya Sheria katika Mkutano Kwanza leo Jijini Arusha
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Mhe. Gasinzigwa Oda kutoka Rwanda akichangia hoja kuhusu Kamati ya Sheria katika Mkutano Kwanza leo Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akinukuu jambo wakati wa Mkutano Kwanza wa (Eala), ukiendelea leo Jijini Arusha
Mbunge wa Eala kutoka Sudan Kusini Mhe. Mukulia Kennedy Ayason akichangia hoja kuhusu Kamati ya Sheria katika Mkutano Kwanza leo Jijini Arusha
Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kanda wa Kenya, Adan Mohamed (kulia) akijadili jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) nje ya Ukumbi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala), mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Kwanza, Kikao cha tano, Bunge la nne, ulioanza leo Jijini Arusha.
***********************
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala) limeanza leo mkutano wake wa kwanza, kikao cha tano, bunge la nne ambapo pamoja na mambo mengine, Bunge hilo limejadili masuala mbalimbali ya kamati ya sheria na maendeleo yake ndani ya Jumuiya hiyo.