Mkurugenzi Chuo Kikuu Huria Kituo cha Morogoro, Dkt Wambuka Rangi, akizungumza na wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari ya Elu ya mjini Morogoro (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.
Mkurugenzi Chuo Kikuu Huria Kituo cha Morogoro, Dkt Wambuka Rangi, akifurahi pamoja na wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari ya Elu ya mjini Morogoro (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.
…………………………………………………………………………
NA VICTOR MAKINDA: MOROGORO
Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na watoto wa kike kote nchini katika dhana ya kujitambua, kujiamini sambamba na kuweka na kutimiza malengo.
Hayo yameelezwa jana Octoba 11 na Mkurugenzi Chuo Kikuu Huria Kituo cha Morogoro, Dkt Wambuka Rangi, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari ya Elu ya mjini Morogoro, wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.
“ Dkt Rangi alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni mfano mzuri ambao watoto wa kike kote nchini wanapaswa kuuiga kwa kuwa uongozi wake wenye umakini na weledi mkubwa katika kuliongoza Taifa, unaonesha ni jinsi gani mtoto wa kike akipewa fursa anaweza sawasawa na mtoto wa kiume.
“Umakini, umadhubuti na kiwango kikubwa cha kujiamiani katika kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa, ambako Rais Samia anaonesha ni mfano ambao watoto wa kike wanapaswa kuuiga ili waweze kutimiza malengo yao ya baadae.” Alisema Dkt Rangi.
Dkt. Rangi aliongeza kusema kuwa watoto wa kike wanapaswa kuwa na watu wenye mafanikio ambao watawatumia kama vioo vya kujitazamia na kwa sasa wamtumie Rais Samia Suluhu Hassan, kama kioo cha kujitazamia kuelekea kufanikisha malengo yao.
MWISHO