Habari Picha na / Philemon Solomon
………………………………
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa amesema kupitia
wizara hiyo imeweka mikakati ya kuwajengea uwezo wataalam wake kwa
kuwashirikisha kwenye miradi mikubwa ya ujenzi nchini.
Akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo
na Wakadiriaji Majenzi,uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha, Prof.Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kutumia fursa
waliyonayo kwa kuwajengea uwezo wataalamu wanafunzi.
Aidha amezitaka taasisi zenye mamlaka kuhakikisha wataalam
wanaopewa dhamana ya kutekeleza miradi wanazingatia sheria katika upatikanaji
na uendeshaji wa ujenzi ambapo amewataka wataalamu hao kuwa waadilifu na
wazalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Kwa upande wake rais wa Chama cha Ubunifu Tanzania na Chama cha
Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe katika mkutano huo amesema kuwa
changamoto kubwa waliyonayo ni ushirikishwaji Mdogo wa Sekta binafsi katika
miradi ya serikali.
Naye Msajili wa Bodi ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi Arch.Edwin
Nnunduma amesema hadi kufikia septemba mwaka huu jumla ya wataalam 1188 na
makapuni 411 yamesajiliwa na kuwafuta wataalam 132 na Makampuni 72 kutokana na
makosa tofauti tofauti.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Pro.Makame Mbarawa akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Bodi ya Usajili
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu
wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Msajili wa Bodi ya Wabunifu majengo
na Wakadiriaji majenzi Arch.Edwin Nnunduma akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe: Pro.Makame Mbarawa.
Chama cha Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe akitoa hotuba yake
wakati wa mkutano huo.
Seemu ya washiriki wa mkutano
wakifuatilia mada mbali mbali.
Uchukuzi Pro.Makame Mbarawa akiangana na watumishi wa Bodi ya Wabunifu
majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) alipotembelea banda hilo kujionea shughuli zinazofanywa na bodi hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Pro.Makame Mbarawa akisalimiana QS. Bundala Mashaka alipowasili kufungua
mkutano wa wataalamu wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
AICC Arusha. (wa kwanza kushoto) Msajili wa Bodi hiyo Arch.Edwin Nnunduma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Pro.Makame Mbarawa akisalimiana na Rais wa Chama cha Ubunifu Tanzania na Chama
cha Ubunifu majengo Afrika Mashariki David Kibebe alipowasili kufungua mkutano
wa wataalamu wa sekta ya unjenzi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano AICC
Arusha.
yao kabla ya kuingia katika mkutano.
—