Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga katika aliyekaa akiwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa pamoja wakiwa kwenye picha wakati wa kutoa taarifa kwa UMMA juu ya kongamano la uwekezaji sekta ya misitu mkoa Iringa
********************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni wa Heshima katika kongamano la uwekezaji katika sekta ya misitu mkoani Iringa Litakalofanyika mwezi ujao mkoani Iringa kuanzi 10 hadi 12 kwa lengo kuchochea uwekezaji nchini
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa kikao cha maandalizi ya kongamano hilo amesema, hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan lililosisitiza utumiaji wa malighafi zilizopo kuanzisha na kuchochea maendeleo ya viwanda
Mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na misitu ya kupandwa yenye eneo la hekari la takribani 325,00 na zaidi ya asilimia 40 ya eneo hilo linapatikana mkoani Iringa kutokana na hali ya hewa nzuri iliyopo inayosababisha ukuaji mzuri wa miti ya kupandwa.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa umefanikiwa kuwavutia wawekezaji wengi wa upandaji miti,uchakataji na watoa huduma wa sekta ya misitu hivyo mkoa wa Iringa unakiu kubwa kuona uwekezaji wa misitu unakuwa kwa kasi kubwa na kuchangia zaidi pato la taifa na kwa sasa misitu inachangia kwa asilimia 75 ya mapato ya mkoa wa Iringa.
Sendiga alisema kuwa thamani ya sekta ya misitu bado uko chini ukilinganisha na fursa zilizopo katika uwekezaji mzima ambao umejikita katika uzalishaji wa mbao,nguzo pamoja na bidhaa zilizohandisiwa (engineered wood products) kama vile plywood.
Aliongeza kuwa kuna fursa zaidi kama utengenezaji wa viberiti,toothpick, karatasi,samani zenye ubora unatakiwa kitaifa na kimataifa,uchataji wa mbao ambao umekuwa unafanyika kwa teknolojia duni hivyo kuna fursa za kuuza mashine zenye teknolojia kubwa ama teknolojia mbadala ya bidhaa za misitu.
Sendiga alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa imejipanga kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara hasa ya vijijini ambako shughuli za mazao ya misitu kwa kiasi kikubwa yanapatikana huko.
Alisema kuwa anawakaribisha wawekezaji kwenda mkoa Iringa kujifunza kwenye fursa zilizopo kama vile fursa za uwekezaji katika uazalishaji wa karatasi nyeupe,karatasi za vifungashio,veneer,marine boards,MDF,particle boards,wood chips,block boards na bidhaa nyingine zinazotokana na zao hilo.
Sendiga alisema kuwa kongamano hilo latafanyika kwa ushirikiano wa taasisi zinazojihusisha na shughuli za misitu kama vile taasisi ya uwekezaji misitu Tanzania (forestry development trust),mradi wa panda miti kibiashara awamu ya pili pamoja na wadau wengine wa sekta ya misitu.
Alisema kuwa kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 12 mwezi wa kumi na moja katika viwanja vya shule ya msingi Wambi mjini Mafinga na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa atakaye fungua kongamano hilo na kongamano hilo litakuwa endelevu na kufanyika kila mwaka.
Sendiga alimalizia kwa kusema kuwa kongamano hilo linatarajia kuwaleta kwa pamoja wadau wote wa sekta ya misitu,taasisi na wizara zinazohusika na misitu na uwekezaji (TAMISEMI,Wizara ya Maliasili na utalii,wizara ya uwekezaji,wizara ya viwanda na baishara,kituo cha uwekezaji,wazalishaji na wasambazaji wa teknolojia za uchakataji wa mazao ya misitu,taasisi za elimu ya misitu,wadau katika sekta ya usafirishaji,taasisi za fedha na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani katika sekta ya misitu.
Kwa upande wake Elisha Edison mwekezaji wa kiwanda cha Agola wood products limited alisema kuwa wamewekeza kwenye kuzalisha bidhaa za mbao kama ambavyo wanavyofanya hivi sasa kwa kujenga nyumba kwa kutumia mbao ambazo zimekuwa zinatumia gharama ndogo na zinadumu kwa miaka mingi.
Alisema kuwa anawakaribisha wananchi kujifunza ujenzi wa nyumba za mbao ambazo zimekuwa zinatumia gharama nafuu tofauti na ujenzi nyumba unaotumia mchanga,saruji,tofari hivyo mazao ya misitu yanamchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa.
Edison alisema kuwa nyumba hizo kipindi cha majira ya joto huwezi kulisikia joto hilo na wakati wa baridi sana napo huwezi kusikia baridi kutoka na malighafi ambazo wanazitumia kujenga nyumba hizo zinzkuwa kwenye ubora wa hali ya juu sana.
Alisema kuwa ni moja ya nyumba ambayo unaweza kuibadili muonekano unavyotaka kutokana na aina ya malighafi ambazo zimetumiwa kujenga nyumba hizo.
Edison alisema kuwa changamoto ambayo wanakumbana nayo ni zao la misitu kutotambulika kama ilivyokuwa sekta nyingine kama sekta ya kilimo na maji wakati vyote hivyo vinabebwa na zao la misitu kwa kuwa kilimo kinategemea misitu kupata mvua na hivyo hivyo vyanzo vya maji vinatunzwa na misitu.
Lakini pia Edison aliiomba serikali kuingalia sekta ya misitu na kuipunguzia utitili wa kodi uliopo katika mazao ya misitu ambayo kwa sasa inachangia zaidi ya asilimia 70 ya pato la mkoa wa Iringa.
Nao wakuu wa wilaya ya Iringa walisema kuwa wanawakaribisha wawekezaji wa mazao ya misitu kwa kuwa fursa hiyo ipo na kuna maeneo mengi ya ukezaji katika wilaya zote za mkoa wa Iringa.