Afisa mwandamizi wa mauzo na masoko kutoka shirika la nyumba la Taifa(NHC) , Tuntufye Mwambusi akizungumza kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo katika shirika hilo jijini Arusha (Happy Lazaro)
…………………………………………………………………
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Shirika la nyumba la Taifa (NHC) limewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za nyumba nzuri na za kisasa zilizopo katika shirika hilo huku nyingine zikiendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Afisa mwandamizi wa mauzo na masoko kutoka shirika hilo,Tuntufye Mwambusi wakati akizungumzia fursa mbalimbali zilizopo katika shirika hilo.
Amesema kuwa, kwa mkoa wa Arusha wana mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi katika mji wa Safari City lililopo eneo la Kisongo ambapo nyumba hizo zimepangwa vizuri huku zikiwepo huduma zote muhimu za kijamii zinazohitajika.
“Kwa kweli sisi Kama shirika la nyumba tumekuwa tukihakikisha miji yetu inapangwa vizuri kwa kujenga makazi bora na yaliyopangwa vizuri na mbali na kuwapangishia wateja wetu pia tumekuwa tukiuza nyumba kwa punguzo kubwa la bei huku mteja akiwa na nafuu ya kulipia kwa awamu .”alisema Tuntufye.
Amesema kuwa,waliweza kujenga nyumba za mfano na nyingine waliuza kwani wana punguzo la asilimia 40 kwa sasa hivi ,hivyo aliwataka wananchi katika mikoa mbalimbali kuchanganya fursa hiyo .
Amefafanua kuwa,wameleta mradi huo wa Safari City kwa sababu wanaelewa changamoto ya mipango miji katika jiji letu ,hivyo wakaamua kuja na mradi huo ambao ni mfano wa kuigwa kwani umepangwa vizuri huku huduma zote za kijamii zikipatikana kwa urahisi.
Tuntufye ameongeza kuwa, wana mradi wa ujenzi wa nyumba Dodoma ambapo wanajenga makazi elfu Moja na wanatarajia kuzindua hivi karibu huku akisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu Sana na Serikali na wataweza kuuza hizo nyumba pia.
“Kwa mkoa wa Arusha hapa mtu unaweza kuweka uwekezaji mkubwa kwani Kuna fursa kubwa Sana za kibiashara ndio maana na sisi tunaendelea kuwekeza zaidi ili kuwarahisishia huduma wateja wetu na kuwaletea huduma kwa karibu zaidi.”amesema.
Aidha Tuntufye aliwataka watanzania watumie fursa katika kuchukua nyumba hizo za shirika la nyumba zilizopo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuweza kupata huduma nzuri zaidi.