******************************
Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, amewahakikishia wakazi wa Visegese ,kuwa barabara ya Chamgoi -Vianzi -Visegese yenye km.15 inakwenda kuboreshwa katika bajeti ya mwaka 2022-2023 kupitia wakala wa barabara vijijini TARURA.
Akizungumza na wakazi wa kata:-ya Visegese na Mkamba kwenye vijiji vya Visegese,Kikundi ,Kizomla na Kibunguchana kwenye ziara yake ya Jimbo alisema, barabara hiyo bado ni kero kwa wananchi kwa kipindi kirefu sasa.
“TARURA ijitoe kuhudumia wanyonge kwa kufika kuona maeneo ya vijijini ili kujua changamoto na kuweza kuzitatua ,na kufungua barabara hii nawaomba TARURA wafike na huku waone watu wanavyotaabika”
“Sisi Mkuranga tumepata bilioni 2.6 ,za kuimarisha barabara zetu za vijiji, Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,,Samia Suluhu kwa kuzipa vipaombele barabara hizi za ndani ,”alifafanua Ulega.
Ulega alieleza mkakati ni kuimarisha na kufungua baadhi ya barabara ikiwemo Zogowale na pia Kizomla kwa kuweka japo mifereji ambapo imetengwa milioni 120.
Akizungumzia nishati ya umeme alitaka Shirika la umeme (TANESCO ) kushusha umeme shule shule ya sekondari na kwa wananchi wa Visegese,Kizomla,Kikundi na Kibunguchana .
Katika ziara hiyo Ulega amechangia nguvu za wananchi 500,000 na mifuko ya saruji kwa ajili ya nyumba ya mganga katika zahanati ya Visegese iliyojengwa kwa milioni 50.
Vianzi amechangia sh.500,000 na mifuko ya saruji,ujenzi wa zahanati Kizomla saruji mifuko 100 na milioni moja na Kijiji Cha Kikundi kata ya Mkamba kachangia 500,000 na mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati inayoendelea na kijiji cha Kibunguchana sh.500,000 na mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya shule shikizi .
Diwani wa kata ya Mkamba ,Hassan Dunda alisema ipo changamoto kubwa Ni upungufu wa madarasa kwenye shule za msingi, umeme ambapo Mkamba ina vijiji 8 na vijiji sita tayari umeme unavutwa ,tatizo la maji katika vijiji vya Kizomla,Kikundi na Kibunguchana pamoja na baadhi ya miundombinu ya barabara kuwa kero ikiwemo Kihimbwa -Kisapara .
Akijibu suala la umeme meneja TANESCO Mkuranga Theodory Hall alisema wameshaweka vigingi katika baadhi ya vijiji wanatarajia kuweka nguzo .
Alieleza, huko Kigoda ,Kizomla wanapeleka umeme kupitia ujazilizi Mkandarasi ni Sengerema pia Kijiji Cha Kikundi na Kibunguchana wanafikishiwa umeme kupitia mradi wa REA III mzunguko II .
Hall aliwahakikishia umeme kuwaka katika vijiji hivyo mwaka ujao 2022.