Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa China Mhe. Chen Mingjian Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 11 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa China Mhe. Chen Mingjian mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Chen Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 11 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo tarehe 11 Oktoba 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Oktoba 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 11 Oktoba 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mhe. Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, leo tarehe 11 Oktoba 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwaapisha Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mhe. Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, leo tarehe 11 Oktoba 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU