………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ametoa rai mchezo wa bao utukuzwe ili kumuenzi muasisi ,marehemu baba wa Taifa ,hayat Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia 14,oktoba 1999.
Ameeleza ,michezo ya jadi ihakikishwe inafufuliwa nchini kwani Ni kielelezo Cha Taifa.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika fainal ya mchezo wa bao aliyoiandaa ili kumuenzi baba wa Taifa ,Ulega alieleza wapo wadau waliomsaidia kumshika mkono ikiwemo Asas ambao wametoa fulana za washiriki wa timu za bao na amewashukuru wazee maarufu wacheza bao Mkuranga .
Alisema Jambo la kudumisha michezo ya jadi imesisitizwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umuhimu wa kurithisha utamaduni watoto na kama hatuenzi tamaduni zetu zitapotea .
“Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu anahimiza michezo, na kuenzi historia ya jadi sana Zanzibar hawajawahi kuacha jadi yao hata mwaka mmoja ,ambapo kila mwaka kuna maonyesho ya jadi na mwaka huu yeye mwenyewe alikuwa kinara , kwenye michezo hiyo ya jadi maarufu Kama Mwaka kogwa ili kudumisha masuala ya jadi”alisisitiza Ulega.
Pamoja na Hilo ,aliwaasa wananchi kuendelea kudumisha amani na upendo ,kumuenzi baba wa Taifa.
Ulega aliahidi kuendeleza mashindano ya mchezo huo kila mwaka ,ambapo Safari hii alitenga milioni moja kwa washindi watatu ambapo mshindi wa Kwanza Vikindu walipatiwa kikombe na sh.500,000, Mwarusembe washindi wa pili 300,000 na Magawa 200,000 ambao ni washindi wa tatu.
“Washindi Hawa watatu pia nimewaongeza 50,000 kila timu ili kununua bao mpya .”alifafanua Ulega.
Mcheza bao miaka mingi iliyopita Selemani Ndugugani alieleza, Michezo hii ilianza mwaka 1975 na mwaka 1976 alianza kushiriki michezo hii hadi mwaka 1980″
“Michezo hii ya jadi inaonekana kufa lakini tunamshukuru mbunge Ulega kufufua huu mchezo wa bao,:’;”inafaida Kama soka tu miaka hiyo Mimi mchezo huu ulinifikisha mikoani Musoma,Bukoba,Lindi “
Alimuomba Ulega kuzungumza na wizara ya Utamaduni kuenzi michezo hii na sio soka pekee.
Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasir alieleza ,mchezo wa bao unaimarisha akili na kuleta furaha .
“Mwanzilishi wa mchezo huu hayat Mwl.Nyerere alidumisha mchezo huu na sisi tunapaswa kuuenzi “
Mashindano hayo yalianza ngazi za vijiji na kuunda mashindano ya kata hadi Tarafa na kufuzu kuingia robo fainal .