Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akiakivishwa medali baada ya
kumaliza mbilio za Kilometa 10 katika mashindano ya Riadha ya Capital City
Marathon 2021 yaliyofanyika leo Oktoba
10,2021 jijini Dodoma. Mbio za Nyika za Capital City Marathon zilidhaminiwa na
Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akiakimkabidhi zawadi ya kitita
cha Shilingi Milioni moja kwa mshindi za Kilometa 21 wanawake, Failuna Matanga
aliyekimbia kwa Saa 1:20:59 katika Mbio za Capital City Marathon zilizofanyika
leo Oktoba 10,2021 jijini Dodoma. Kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Yessaya Mwakifulefule. NIC ndio wadhamini wakuu wa
mbio hizo.
MASHINDANO ya pili ya Capital
City Marathon 2021, yamefanyika jijini Dodoma leo chini ya udhamini wa Shirika
la Bima la Taifa (NIC) na kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 2,000 kutoka kila
pembe ya nchi.
Wakimbiaji kutoka Arusha na
Singida waling’ara katika mbio hizo na kujinyakulia medali na vitita vya fedha
taslimu.
Washindi wa mbio za 21km upande
wa wanaume ni Josephati Gisemo (01:06:47)-Arusha, Hamisi Athumani (01:06:50) Singida,
Yohan Sule (01:07:12) Arusha, Aloyce Simbo , Agustine Sule, Rashid Muna, Marco
Joseph, Emmanuel Gadiye, Saidi Juma na
Nestory Stivin .
Washindi upande wa wanawake,
Mshindi Matanga (01:20:59), Mery Naali (01:23:02), Tunu Andrea (01:23:11), Sara
Ramadhani, Angel John, Ramla Phabian, Asia Dedu, Visa Mhalwa, Rose Malia na
Shania John.
Washindi wa 10km wanaume ni
Kaposh Laizer (29:03:16), Inyasi Sule (29:11:93) , Fabian Nelson (29:51:23),
Jamali Saidi, Nelson Mbuya, Haji Luli, Elizante Elibariki, Shija Ngelela, Amani
Owen na Bosco Kangalwe.
Washindi wa 10km wanawake ni
Transfora Musa (34:04:02), Anastazia Dolomogo (35:32:23), Aisha Lubuna
(35:53:91), Neema Kisuda, Agnes Protas, Rebeca Bajuta, Neema Sanka, Sarah
Hijti, Anna Rogath na Aisha Mohamed.
Akizungumza leo mara baada ya
kukamilika kwa mbio hizo, mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema
mbio hizo zimeunga mkono jitihada za serikali za katika adhma yake ya
kuhakikisha inapiga vita magonjwa yasiyo ya kuambukiza .
‘’ Nashukuru kwa kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye
anasisitiza wananchi kufanya mazoezi , niwaombe kila mmoja wetu akawe balozi
huko tunakotoka, matukio haya yanapokuwepo mahali yanafanya mambo mengi ikiwemo
lile la afya kwa sisi tuliofanya mazoezi ’’ amesema
Kwa upande wake , Mkurugenzi
wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule ,amesema mbio hizo ni
mbio ambazo hupanda thamani kila mwaka hivyo husaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza
ajira kwa vijana .
‘’NIC tumedhamini mbio hizi kupitia bidhaa
yetu ya Bima ya Makazi tukiwataka
watanzania waweze kulinda makazi yao , hii si mara ya kwanza kwa NIC kushiriki
kwenye michezo mbalimbali kwa maana ya riadha, mpira wa miguu, kwasababu tunaamini
michezo ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na hata serikali yetu
inasisitiza kwamba vijana wajiajiri kupitia michezo’’ amesema
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Michezo Nsolo Mlozi, amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
kufanikisha mazoezi na mazoezi kwani imeweza kurahisisha maisha ya watanzania
kwa kujenga undugu pamoja na urafiki’’ Leo tuko hapa watu takribani elfu mbili
maana yake Dodoma imejengeka kiuchumi’’