*******************************
Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amewahakikishia wakazi wa KondoMwelanzi kata ya Bupu kupata kipaombele Cha kujengewa daraja la mto Kipilimba ili kuondoa kero wanayoipata wakati wa mvua kushindwa kupitika.
Aidha mbunge huyo ameielekeza wakala wa barabara Vijijini (TARURA )wilaya ya Mkuranga kuzipa kipaombele barabara kero Kibudi- Mbulani pamoja na Panzuo shule ambapo wakazi wa Kibudi hulazimika kutumia usafiri wa pikipiki kwenda na kurudi sh.10,000.
Ulega alibainisha hayo katika ziara yake ya Jimbo kata ya Panzuo na Bupu kwenye vijiji vya Mbulani,Tundu,Kibudi,na Kondo Mwelanzi ambapo aliitaka TARURA kuweka ujenzi wa daraja hilo katika bajeti ijayo 2022-2023.
Alieleza ,imeshatolewa milioni 100 kwaajili ya maboresho barabara kuu ya Bupu -Kiparanganda sasa TARURA ifungue na barabara Tundu-Kiziko ,Bupu-Kibudi ,Zogowale kuondoa eneo korofi,ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Ulega aliielekeza pia TANESCO
kufikisha umeme Mbulani-Panzuo kwa wateja walikwishalipia ,zahanati ya Panzuo,sekondari Panzuo,na Shule ya sek Mandikongo na Shule ya msingi Mamrimpera.
Aliwaeleza wananchi wa kata hizo kuvuta subira kwa changamoto ambazo bado zipo kwenye mchakato wa kutatuliwa.
“Serikali ya awamu ya sita inapiga kazi katika sekta zote ,na hadi sasa mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameshatoa tilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15,000 nchi nzima,
“Serikali pia imetenga kiasi cha sh.bilioni 966 kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuboresha barabara pamoja na madaraja maeneo mbalimbali nchini”Yaani Samia anaupiga mwingi ile mbaya ,tumpe ushirikiano na tuendelee kumuamini na kumuunga mkono”alisisitiza Ulega.
Katika ziara hiyo Ulega ametoa mifuko ya saruji 50 na sh.500,000 katika ujenzi wa zahanati Kibudi na pamoja na mifuko ya saruji 50 na sh .500,000 Bupu ujenzi wa zahanati ,500,000 ujenzi wa msikiti ,Tundu ujenzi wa nyumba ya mganga 500,000 na mifuko ya saruji 50,Mbulani mifuko ya saruji 50 na sh .400,000 kwa ajili ya wodi ya wazazi zahanati ya Mbulani na amechangia baadhi ya vikundi vya akinamama ikiwa ni fedha sh 800,000 fedha zake binafsi.
Awali diwani wa kata ya Panzuo Dude Hamis alisema, wanakabiliwa na changamoto ya umeme ambapo nyumba zilizokadiria zilikuwa 125 zilizopata ni 20 pekee licha ya wateja hao kulipia toka Juni mwaka huu huku zahanati wakitumia tochi na vibatari.
Jingine ni shule ya msingi ni ya muda mrefu imejengwa miaka ya 70 ,hawajapata madarasa na yaliyopo ni chakavu , barabara ya Zogowale ni eneo korofi eneo la mlima linahitajika kujengwa mitalo .
Meneja wa TARURA Mkuranga Silas alisema tayari kiasi Cha sh .milioni 120 kipo kwa ajili ya bajeti hii .
Akijibu kuhusiana na ombi la ujenzi wa daraja Dondwe-mto Kipilimba alisema amelipokea na watalipa kipaombele bajeti ijayo .
Nae meneja wa TANESCO Mkuranga Theodory Hall alisema ,baada ya wiki mbili wataanza na zoezi la kuunganishia wale waliolipia Mbulani na kudai baadhi ya maeneo yapo kwenye mpango wa REA na kuwahakikishia umeme kwenye utafika katika maeneo aliyoomba mbunge Ulega ikiwemo shule za sekondari ,msingi na zahanati .
Mwenyekiti wa CCM Mkuranga,Ally Msikamo aliwataka wataalamu watoke maofisini na kwenda maeneo ya Vijijini kujionea uhalisia wa changamoto zinagusa wananchi.