Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (kushoto) akisalimiana leo na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Chacha (kulia) na viongoizi wengine alipowasili kwa ajili ya utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akitoa elimu leo kwa wakazi wa Kijiji cha Mtakuja wilayani Kaliua ya umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Chacha (aliyesimama) akitoa taarifa leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani(mbele aliyekaa) kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa nane wa wizi wa ng’ombe 328 katika Kijiji cha Lumbe na Mpanda Mlowoka.
Picha na Tiganya Vincent
*****************************
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka Wakazi wa Wilaya ya Kaliua kuendelea kuwafichua watu wasio na nia njema kutoka mikoa jirani kuingia na kuendesha vitendo kiharifu.
Alisema kuna baadhi ya waharifu kutoka nje ya Tabora wamekuwa wakishirikiana na wenyeji wenye tabia mbaya na kuendesha vitendo visivyofaa ikiwemo ujambazi na wizi wa mifugo
Balozi Dkt.Batilda ametoa kauli hiyo leo baada ya kupokea taarifa ya hali ya usalama kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Chacha ambayo ilionyesha Polisi walivyofanikiwa kukamata watuhumiwa 8 waliokuwa wameiba ng’ombe 328.
Aliwataka wananchi waendelee kutoa taarifa za Waharifu ili Polisi waendele na juhudi za kutafuta myonyoro wote wa vitendo vya wizi wa ng’ombe na uhalifu mwingine kwa ajili ya wananchi na mali zao ziendelee kwa salama.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Chacha alisema tukio la kwanza lilitokea katika Kijiji cha Lumbe ambapo walikamatwa watuhumiwa 5 wakiwa wameiba ng’ombe 28 .
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mifano silaha ambazo wanachezea Watoto (toy) wakijifanya askari wa wanyamapori na wakiwa wamewaingiza kwenye Pori ng’ombe hao.
Chacha alisema tukio la pili la wizi wa ng’ombe 300 lilitokea katikia Kijiji cha Mpanda Mlowoka ambao watuhumiwa 3 walikamatwa.
Aliisema walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kufuatia ushirikiano kutoka kwa wananchi wa kuwapigia simu na Polisi kukimbia haraka katika eneo la tukio.
Chacha aliongeza kuwa baada ya mahojiano ya kina wamebaini watuhumiwa hao ambao wana nje ya Mkoa wa Tabora wamekuwa na ushirikiano na mkazi mmoja wa Tabora ambaye ndio anawatengenezea mazingira ya kutenda makosa hayo.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano na watuhumiwa na kuendelea kumtafuta mwenyeji wa watuhumiwa ili waweze kufikishwa Mahakamani.