********************************
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe wachangamkia ujenzi kituo cha Afya cha Tarafa ya Mihambwe huku wakimshukuru sana Rais wa Jamahuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kuwapatia fedha Tsh. 250,000,000/= za ujenzi.
“Naipongeza sana Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kutukumbuka na kusikia kilio chetu sisi Wananchi wake tuliokuwa tukipata shida. Sisi tupo pamoja na Rais Samia, tunajitolea sana nguvu zetu kujenga. Ahsante sana Mama.” Alisema Shafii Ibrahim Mtonya mkazi kata ya Mihambwe.
Halikadhalika Mwenyekiti Kijiji cha Mihambwe Ahmad Maliyangu ameonyesha furaha yake namna Serikali inavyoshirikiana nao na kuhaidi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.
“Tunafurahi namna Afisa Tarafa Mihambwe, Shilatu anavyoshirikiana nasi kuhakikisha ujenzi wa kituo cha afya unakamilika. Mwenyezi Mungu azidi kumbariki Rais Samia nasi tupo nyuma yake kila hatua.” Alisema Ahmad Maliyangu.
Hayo yamejitokeza kwenye ziara aliyoifanya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ya kwenda kuungana na Wananchi kushiriki ujenzi kituo hicho cha afya.
“Nimekuja kuungana nanyi kushiri ujenzi natoa rai mjenge kwa kasi, viwango vinavyoendana na thamani ya fedha. Kwa niaba ya Wananchi Tarafa ya Mihambwe tunamshukuru na kumpongeza sana kabisq Rais Samia kutupatia fedha za ujenzi, tunamuhaidi kuendelea kuwa watiifu na kumuunga mkono nyakati zote.” Alisisitiza Gavana Shilatu
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Kamati za ujenzi za mradi huo wa kituo cha afya ambao unahusisha ujenzi wa majengo matatu ambayo ni jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), Maabara na kichomea taka.