Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri (katikati) akikata utepe kuzindua bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Bw.Prosper Kasenegala akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri (kulia) wakipata picha ya pamoja watumishi wa Puma Energy katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wacheza ngoma wakitoa burudani katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited imezindua laini yake mpya ya Vilainishi vyenye kukidhi mahitaji ya magari, Viwanda na mitambo mbalimbali ambayo inauwezo wa kutumika kwa muda mrefu pasipokuwa na usumbufu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah amesema vilainishi hivi sio tu ni bora na vya hali ya juu lakini pia ni utaratibu wa kisasa wa kuchochea tabia mpya ya kuchagua kilicho bora zaidi.
Aidha Bw.Dhanah amesema kuwa Vilainishi hivyo vimetengenezwa na kuratibiwa nchini Uswizi kwa kuzingatia matakwa na ubora wa viwango vya kidunia na nchini kwa ujjumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri amesema Puma Energy itawekeza zaidi ya dola Milioni 100 (Takribani Bilioni 230) katika miaka 3 ijjayo nchini Tanzania, uwekezaji huu nia katika mwendelezo wa jitihada za kampuni kufikia jamii na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta na vilainishi kwa bei nzuri na kiwango sahihi katika nchini.
“Tungependa kuwaalika wateja wetu wanaothaminiwa, kubadilisha machaguo yao na kuchagua Oili na Vilainishi chapa ya Puma energy kwani ni aina mpya ya vilainishi vinavyo kuhakikishia ulinzi na ubora wa injini yako”. Amesema Bw.Mitri.
Nae Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Bw.Prosper Kasenegala amewasihi watanzania kutumia vilainishi vya Puma na kusisitiza kuwa Oil na vilainishi hivyo sasa yanapatikana katika vituo vyote vya Puma Energy nchini kote na kwamba ni kipaumbele cha kampuni hiyo kuhakikisha vilainishi vyenye ubora vinapatikana kwa wateja wao katika muda wote.