Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida Oscar Kalimilwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.hususani hatua ya mfuko huo kutoa msamaha kwa waajiri wote wenye malimbikizo ya michango na tozo itokanayo na ucheleweshaji wa michango kwa kuzingatia vigezo
Afisa Huduma kwa Wateja NSSF Mkoa wa Singida, Latifa Singano akimpatia vipeperushi mteja baada ya kupata huduma.
Mhasibu wa NSSF Mkoa wa Singida Keneth Kalinjuma akizungumzia msamaha wa tozo uliotolewa kwa waajiri ambapo msamaha huo ulioanza Oktoba Mosi imeelezwa kwa waajiri watakaofanikiwa kulipa malimbikizo ya michango na tozo inayoishia Juni 30, 2021 kwa kuilipa hadi ifikapo Novemba 30, 2021 watasamehewa kwa kiwango cha asilimia 100. Pia watakaolipa ifikapo Desemba 31, 2021 watapata msamaha kwa kiwango cha asilimia 75 huku watakaolipa ifikapo Januari 31, 2022 watasamehewa kwa kiwango cha asilimia 50.
Afisa Mafao wa NSSF Mkoa wa Singida Mwajuma Juma akizungumza na waandishi wa habari.kwenye wiki ya huduma kwa wateja ambapo alihamasisha wananchi kujitokeza kutembelea ofisi hizo ili kunufaika na fursa mbalimbali,
Wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Singida wakifurahia maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.
Kazi ikiendelea.
Kazi ikiendelea.
Wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wao Oscar Kalimilwa (katikati) (Picha zote na Dotto Mwaibale)