Wafanyakazi wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga wakigawa vyakula kwa wateja wa Benki ya TCB ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga, imeadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja kwa kupata kifungua kinywa (chai) pamoja na wateja wao ili kufurahi nao pamoja.
Wafanyakazi wa Benki ya TCB wamekunywa chai na Wateja wa Benki hiyo leo Alhamis Oktoba 7,2021 ndani ya Benki ya TCB (iliyokuwa Benki ya TPB) ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja mwaka 2021 yenye kauli mbiu ya Nguvu ya Huduma (The Power of Service).
Wafanyakazi wa benki ya TCB tawi la Shinyanga wakiongozwa na Meneja wao Julius Mataso wametoa huduma ya chai kwa wateja wao ambapo kesho watakata keki ya pamoja.
Akizungumza na wateja wao huku wakiendelea kupata kifungua kinywa, Meneja wa benki hiyo Tawi la Shinyanga Julius Mataso amesema katika wiki hii ya huduma kwa wateja, wameona ni vyema wakapata chai ya pamoja na wateja wao ili kufurahi pamoja na kuonyesha namna benki ya TCB inavyowajali wateja wake.
“Wiki hii ni ya huduma kwa wateja, na sisi bila nyie hakuna chochote, hivyo Benki yetu itaendelea kuwathamini wateja pamoja na kuwahudumia vizuri, ambapo pia katika huduma zetu za mikopo tumepunguza riba, hii ni kuonyesha kiasi gani tunavyowapenda wateja wetu,” amesema Mataso.
Aidha, amesema pia wameendelea kuboresha utoaji wa huduma zao kwa wateja zikiwemo za mfumo wa kidigitali ambapo mteja anaweza kutoa pesa zake kupitia simu za kiganjani na hata kutuma au kupokea fedha nje ya nchi kwa njia ya Western Union.
Amesema pia wanatoa huduma za Mawakala, bima za maisha, bima za mali kama vile magari, nyumba pamoja na bima ya mshike mkono kupitia mfumo wa vikundi kwa kutoa fedha ya pole pale mwanakikundi anapopata matatizo ya msiba.
Mataso amesema ili kupata bima ya maisha kupitia Benki ya TCB hakuna haja ya kujaza fomu ya kujiunga kwani ukishakuwa tu akaunti ya TCB basi unakuwa tayari na sifa za kupata huduma hiyo.
Amewaomba Watanzania kuchangamkia huduma ya Akaunti ya Muda Maalumu ‘Fixed Depost Account’ inayotolewa katika Benki ya TCB ambayo wanatoa riba ya asilimia 11 kwa mwaka.
Mataso amezitaja huduma zingine ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbalimbali kama vile mikopo ya watumishi, wastaafu, wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa.
Meneja huyo, aliwahakikishia wateja wa Benki hiyo ya TCB, kuwa wataendelea kutoa huduma bora kwao, na pale penye changamoto wasisite kuwapatia ushauri, ili warekebishe mapungufu hayo, kwani hiyo ni benki yao na ipo kwa ajili ya Watanzania.
Nao baadhi ya wateja wa Benki hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake wafanyabiashara Shinyanga Joyce Egina na Donald Nyerere wameipongeza Benki ya TCB kwa huduma zake ambazo wanazitoa kwa wananchi, na kuwashauri waendelee na kasi hiyo hiyo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza leo Alhamis Oktoba 7,2021 wakati Benki hiyo ikisherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wateja wao. Picha na Kadama Malunde na Marco Maduhu
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akimpatia vitafunwa mteja wa TCB Bank
Wateja wateja wa Benki ya TCB wakichukua chai ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja
Wafanyakazi wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga wakigawa vyakula kwa wateja wa Benki ya TCB ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja
Wafanyakazi wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga wakigawa vyakula kwa mteja wa Benki ya TCB ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja

Kulia ni Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na TCB Bank wakati Benki hiyo ikisherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wateja wao
Kushoto ni Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na TCB Bank wakati Benki hiyo ikisherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wateja wao
Wateja wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga wakipata chai ndani ya Benki ya TCB ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja
Kulia ni Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na TCB Bank wakati Benki hiyo ikisherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wateja wao
Mteja wa Benki ya TCB , Donald Nyerere akiipongeza Benki ya TCB kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Shinyanga (TWCC), Joyce Egina akitoa neno la shukrani kwa Benki ya TCB kwa huduma inazozitoa.
Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kuhudumia wateja wake wakati Benki hiyo ikisherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Picha na Kadama Malunde na Marco Maduhu