Na Mwandishi Wetu – Dodoma
Katika
kutekeleza agizo la Serikali linalowataka wakulima wote
wanaojishughulisha na shughuli za kilimo cha umwagiliaji kuachangia
asilimia tano katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha Umwagiliaji, Tume
ya taifa ya Umwagiliaji imekamilisha Miongozo kanuni na taratibu za
ukusanyaji wa tozo za Kilimo cha Umwagiliaji.
Hayo yamesemwa
Mapema Leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari
ofisini kwake.
Bw. Kaali alisema mapema mwezi July Mwaka huu
Serikali kupitia Waziri wa Fedha ilitoa agizo ya wakulima waliyopo
katika skimu za kilimo cha umwagiliaji kuchangia asilimia tano kwa kila
hekta na fedha hizi ziingizwe katika mfuko wa umwagiliaji kwa ajili ya
kugharamia matunzo, matengenezo pamoja na uendeshaji wa skimu za kilimo
cha umwagiliaji.
Aidha Mkurugenzi Kaali amesema kuanzia mwezi
huu wa kumi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaanza kampeni maalum ya kutoa
elimu kuhamasisha wananchi mbali mbali wachangie watoe hizi ada kwa
ajili a kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, “Hivyo watumishi mbalimbali
kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na viongozi mbali mbali wa serikali
watakwenda katika maeneo mbalimbali ya nchi,kwa ajili ya kuelemisha na
kuhamasisha utoaji wa ada hizi za umwagiliaji.” Alisema Kaali
Bw.
Kaali wamewaasa wakulima wanaojihusisha na kilimo cha Umwgiliaji
kuchangia ada za umwagiliji kwani amesema ni fursa nzuri ssaa ambayo
imetolewa na Serikali kuchangia fedha katika mfuko wa umwagiliaji ili
kuweza kutatua changamoto kubwa katika skimu mbalimbali hapa nchini.
Kwa
pande wake Kaimu Mkurugenzi uendeshaji Bwana Enterbet Nyoni amesema
katika skimu za kilimo cha umwagiliaji zisozendelezwa mgawanyo wa Ada ya
tozo ya asilimia tano ya tozo, utahusisha asilimia sabini na tano (75%)
kubakia katika skimu husika na asilimia ishirini na tano (25%)
itakwenda katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana
na uchangiaji wa Tozo katika sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji.