Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kushoto akizungumza Jambo na makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Mussa Ndomba kuhusiana na mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa kata ya Sofu.
**********************************
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amechangia kiasi Cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Sofu iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha.
Hayo yamebainishwa na Mbunge hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata ya Sofu yenye lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Koka katika ziara hiyo ambayo ameambatana na viongozi mbali mbali wa Chama sambamba na wakuu wa idara na viongozi wa taasisi ametumia fursa ya ziara hiyo kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
“Leo nipo naendelea na ziara yangu katika kata ya Sofu na nimebahatika kutembelea baadhi ya miradi yetu ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari n msingi pamoja na ujenzi wa zahanati ambayo itakuwa na adhi ya kituo Cha afya,”alisema Koka.
Pia Koka alibainisha kuwa anatambua Kuna baadhi ya wanafunzi wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa hivyo mradi huu utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watoto wetu.
Aidha alisema lengo lake kubwa kwa kushirikiana na serikali ni kuimarisha zaidi kuboresha miundombinu mbali mbali ya majengo ya wanafunzi pamoja na madawati ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafika.
Koka aliongeza katika kata ya Sofu Kuna baadhi ya changamoto mbali mbali katika sekta tofauti hivyo atahakikisha anasimamia vizuri ili kuweza kuzitatua changamoto hizo.
Katika hatua nyingine Koka alibainisha kuwa kwa Sasa Kuna ugonjwa hatari wa Uviko 19 hivyo wananchi waondokane na hofu na badala yake amewahimiza kuzingatia maelekezo ya wataalamu ikiwemo kuchoma chanjo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha Mussa Ndomba alisema kutokana na mchango wa Mbunge hiyo wameamua shule hiyo pindi itakapokamilika itapewa jina la Koka secondari .
Ndomba alisema kuwa Koka amekuwa mstari wa mbele katika kuchagiza suala zima la maendeleo katika sekta mbali mbali hivyo umuhimu wake katika jamii ni mkubwa Sana.