Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi,akizungumza wakati akifungua warsha kwa watoa huduma za Posta Kuadhimisha wiki ya Posta Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasailiano Tanzania (TCRA) iliyofanyika leo Oktoba 7,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani ) wakati wa warsha kwa watoa huduma za Posta Kuadhimisha wiki ya Posta Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasailiano Tanzania (TCRA) iliyofanyika leo Oktoba 7,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi (hayupo pichani ) wakati akifungua warsha kwa watoa huduma za Posta Kuadhimisha wiki ya Posta Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasailiano Tanzania (TCRA) iliyofanyika leo Oktoba 7,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk. Jabiri Bakari,akizungumza wakati wa Warsha kwa watoa huduma za Posta kuadhimisha wiki ya Posta Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyofanyika leo Oktoba 7,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi,amesema kuwa jumla ya halmashauri 21,tayari zimefikiwa na huduma ya anuani za makazi huku kazi ya kufikisha na kuunganisha nchi nzima kwa mfumo huo ikiendelea.
Hayo ameyasema leo Oktoba 7,2021 jijini Dodoma wakati akifungua warsha kwa watoa huduma za Posta Kuadhimisha wiki ya Posta Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasailiano Tanzania (TCRA).
Dk.Yonazi amesema kuwa wanaendelea na jitihada za kuweka anuani za makazi nchi nzima ili kurahisisha utoaji wa huduma za usafirishaji mizigo na vipeto.
“Posta ni sekta muhimu sana inawezesha bidhaa moja kutoka sehemu moja
mpaka nyingine na usafirishaji wa mizigo bado unabaki kuwa ni kitu
muhimu Serikali imefanya jitihada kubwa na imewekeza kuhakikisha
miundombinu inakuwa rafiki.
“Na tumeweka Postikodi katika Halmashauri 21 na mipango inaendelea
kuendelea kuweka katika maeneo mengine hii itasaidia mizigo kufika
kila mahali,”amesema Dk.Yonazi
Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtaa, nyumba, njia na barabara zinatambulishwa kwa anuani maalum chini ya utaratibu wa Post code, ili kurahisisha utambuzi na utoaji huduma za Posta nchini.
“Pia utatumika katika utoaji wa huduma nyingine za jamii zikiwemo huduma za kutoa taarifa kwa zima moto, polisi nakadhalika”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk. Jabiri Bakari
amesema kuwa warsha hiyo ni muhimu kwani watoa huduma hao wamekuwa wakitoa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka eneo moja mpaka jingine.
Aidha amesema kuwa TCRA imejidhatiti kuhakikisha huduma za Posta zinakuwa zenye ushindani kwa kuongeza ufanisi.
”Kwa kutumia mkutano huo watajadiliana ni changamoto zipi wamekuwa wakikutana nazo na kisha kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza ufanisi katika eneo la posta”amesema Dk.Bakari
Awali Mkuu wa Kitengo cha Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Haruni Lemanya, akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo ameeleza umuhimu wa watoa huduma za posta hasa wanaosafirisha vifurushi na vipeto kuhakikisha wanatumia mbinu za kisasa na zenye weledi wakati wote.