Naibu katibu Mkuu wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt..Jim Yonazi akizungumza katika Mkutano baina ya Serikali, Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri -AFASU uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini -TIC Dkt. Maduhu kazi akizungumza katika Mkutano baina ya Serikali, Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri -AFASU uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) leo Jijini Dar es Salaam.Wawekezaji na wadau mbalimbali wakiwa katika Mkutano baina ya Serikali, Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri -AFASU uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na Nchi mbalimbali katika kukuza sekta ya viwanda, uzalisha wa vifaa vya tehama lengo likiwa ni kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika mkutano baina ya serikali, wawekezaji pamoja na wafanyabiashara kutoka Nchini Misri -AFASU, Naibu katibu Mkuu wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Dkt..Jim Yonazi amesema ushirikiano huo utasaidia kusogeza uchumi wa kidigitali.
Amesema Serikali imekuwa ikijitahidi kuwajengea mazingira mazuri wawekezaji ambao wamekuwa na uhitaji wa kuja kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini -TIC Dkt. Maduhu kazi amesema wawekezaji hao wanatarajia kuwekeza katika sekta 16 ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo, Utalii pamoja Gesi.
Ujio wa wawekezaji pamoja na wafanyabiashara hao ni matokeo chanya ya ziara iliyofanywa mwezi Juni mwaka huu na kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC Nchini misri ambapo takribani wafanyabiashara na wawekezaji 150 walifikiwa na kituo hicho.