Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hadji Malela anayetumia jina la kisanii Young king
…………………………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hadji Malela anayetumia jina la Young king anayewakilisha Vizuri Mitaa ya Kanyenye,Mkoani Tabora na kanda ya ziwa anatarajia kuachia album yake ya kwanza ya itakayokuwa na jina la The Return of Young king mwishoni mwa Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa katika viwanja vya Ccm wilaya ya Tabora mjini, Young King alisema kwamba album hiyo inatayarishwa na Gkifaa Kutoka Hitimisho Records ,ambayo ni Lebo anayotokea ni moja kati wanachama wanaotengeneza kundi la hitimisho Squad lenye wanachama 5. Wanaowakilisha mkoa wa Tabora.
Msanii huyo alisema baada ya ukimya wa muda mrefu ameachia wimbo wa “TUNAKIWASHA” wenye mahadhi ya HIP HOP unaofanya vizuri kwa sasa katika vituo mbali mbali vya redio na Runinga nchini.
Young king alisema video hiyo imetayarishwa na Outline Media na kusambazwa na Digital Flava Magazine inayosimamiwa na Romeo Savage ambaye ni mmoja kati ya wanachama wa hitimisho Squard.
Aidha Young King alishawahi kufanya vizuri kwenye nyimbo ya Mzigo Ufike, Burn Mashada,Hitimisho Cypher na zingine nyingi zilizomfanya apate mialiko mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Hata hivyo msanii Young King alishawahi Kushiriki Matamasha mbalimbali ikiwemo Fiesta
Msanii huyo mbali na kazi yake , alisema
ni ngumu Kwa Msanii mwingine Kufanya kazi hiyo ya sanaa na biashara hasa akiwepo Mkoani Tabora.
“Nasema kitu kinacholazimu wasanii wengi kukimbilia jijini dar ambako kuna makampuni mengi yanayojihusisha na kazi za sanaa, kitu kinacho sababisha mkoa wa Tabora kubaki bila wasanii” Young King alisema.
Alisema kuwa kwa wasanii waliokwishapiga hatua kidogo ,wamekuwa hawaonyeshi njia kwa wasanii wanaochipikia.
Young King alisema kwamba kwa upande wa vyombo vya habari sapoti yao imekuwa ndogo katika habari za sanaa mkoani Tabora, hivyo aliwaomba kuwasaidia katika kuwatangaza ili wapate wadau wa kiwaendeleza.
Kutokana na changamoto wanazokumbana nazo ni waandishi wa habari kutowatangaza wasanii wameishia kufanya muziki wa mitaaani.
Changamoto nyingine ni mapromota na wamiliki wa kumbi za starehe wamekuwa hawawatumii wasanii wa nyumbani katika matamasha yao,hivyo kufifisha ndoto za wasanii hao.
Msanii huyo amewataka watanzania wote wasapoti kazi zangu kwani ujio wa sasa amejipanga kuanzia utayarishaji wa nyimbo mpaka video. hasa katika ubora wa utayarishaji, “TUNAKIWASHA “ nyimbo 8 zitafuata ,kwa awamu ,zikiwa zinatoka kweye albam hii imayotarajiwa kutoka hivi karibuni .
Alisema katika album hiyo maandalizi yamekwisha kamilika. na kazi zake zinapatikana kupitia mitandao mbalimbali inayosambaza muziki mtandaoni , jina analoitumia ni “YOUNG KING” Kwenye mtandao wa Youtube, Facebook na Instagram Kwa Jina la @Youngkizzohadji , @Digitalflavamag.