Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakifuatilia semina kusu masuala ya umuhimu wa maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Balozi Adadi Rajab akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kujadili namna walipofikia katika suala la maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Afisa miradi TAWLA, Bi.Mary Richard akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kujadili namna walipofikia katika suala la maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Afisa miradi TLS, Wakili Mackphason Buberwa akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kujadili namna walipofikia katika suala la maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Mdau wa Usalama Barabarani, Wakili Jones John akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kujadili namna walipofikia katika suala la maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakifuatilia semina kusu masuala ya umuhimu wa maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakifuatilia semina kusu masuala ya umuhimu wa maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam..Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakifuatilia semina kusu masuala ya umuhimu wa maboresho ya Sheria ya Usalama barabarani uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kulingana na takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) watu takribani Milioni 1.35 hufariki kila mwaka kutokana na ajali barabarani vilevile hugharimu nchi husika karibu asilimia tatu ya pato la taifa na asilimia 93 ya ajali hizo hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati ikiwemo Tanzania.
Ameyasema hayo jana Mkurugenzi mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) Wakili Tike Mwambipile mara baada ya kukutana pamoja na wadau wake kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maboresho ya sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973.
Akizungumza katika mkutano na waandiishi wa Habrai Jijini Dar es Salaam, Wakili Mwambipile amesema mtandao wa asasi za kiraia zinazoshawishi maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani umekuwa unashawishi maboresho katika maeneo makuu sita kama Mwendokasi, Matumizi ya vizuizi vya watoto, Matumizi ya kofia ngumu, Matumizi ya mikanda, Matumizi ya Vilevi na Matumizi ya vifaa vya kielektoniki ili kuweza kupunguza athari za ajali barabarani.
Aidha ameipongeza Serikali kupitia taasisi zake kwa jitihada inayoonesha katika kudhibiti ajali pamoja.
“Tunayo matarajio ya kuwepo kwa maboresho ya sheria ya Usalama Barabarani. HIvyo basi, tunaomba waandishi wa Habari na vyombo wanavyoviwakilisha kuendelea kuelimisha umma juu ya mambo ambayo yanatarajiwa, ili kuwandaa wananchi kuweza kushiriki katika kutekelezeka kwa masuala hayo pindi mabadiliko hayo ya sheria yatakapokuwa yamepitishwa”. Amesema