********************************
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekabidhi mchango wa Shilingi Milioni kumi (Tsh: 10,000,000/-) kwa Wananchi wa Kijiji cha Kifunda Kilichopo Halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kifunda zilizotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Agosti 2, 2021
Akikabidhi fedha hizo, Dkt. Tulia amesema>>>”Ndugu zangu wana Kifunda, mtakumbuka siku kadhaa zilizopita Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa alikuja kuzindua chuo cha VETA na mimi nikamuomba atusaidie kukamilisha ujenzi huu wa kituo cha Afya na hapohapo akatoa maagizo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI lakini pia yeye binafsi akaahidi kutuchangia Shilingi milioni kumi ambazo tayari zimeshafika” -Dkt. Tulia Ackson
“Tunakila sababu ya kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Mama yetu Samia Suluhu Hassan, Rais wetu, kwa namna inavyotuthamini Wananchi wake. Tofauti ya mchango huu uliotolewa na Waziri Mkuu lakini Serikali tayari imeshatoa maelekezo ya kuhakikisha kituo chetu hiki kinamalizika na sisi Wananchi kuanza kupata huduma hapa haraka iwezekanavyo, Jamani tunataka nini tena zaidi kutoka kwa Rais wetu mpendwa?” -Dkt. Tulia Ackson
“Niwaambie tu watu wa Kifunda, Nitahakikisha Mimi pamoja na Mbunge wa Jimbo hili Mhe. Fredy Mwakibete tunasimamia kwa nguvu zote zoezi la ujenzi wa Kituo hiki cha Afya unakamilika kwa haraka chini ya Serikali yetu pendwa”-Dkt. Tulia Ackson