Meneja wa Shamba la mbegu bora za kilimo ASA Wilayani Nzega mkoani Tabora Jacob Chiwanga anayeonekana kwenye picha akishuhudia upakuaji na upakiaji wa mbegu kwenye kituo cha Reli cha Tabora.
Baadhi ya wababemba mizgo wa kituo cha Reli mkoani Tabora wakishusha na kupakia kwenye gari la Mnunuzi John Songo Tayari kwa safari ya kuelekea wilaya ya Nzega mkoani hapa.
Wanunuzi na Maafisa wa wakala wa mbegu bora za kilimo wakishuhudia upakuaji na ubebaji wa mpenbejeo katika kituo cha Reli mkoa Tabora.
…………………………………………………………….
Na Lucas Raphael,Tabora
Wakala wa mbegu bora za kilimo nchini ASA imesema kwamba msimu wa kilimo 2021/2022 imekusudia kusambaza tani 500 za mbegu bora za mahindi kwa kanda ya ziwa na Magharibi .
Kauli hiyo ilitolewa jana na meneja wa shamba la mbegu bora za kilimo la Kilimi wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jacob Chiwanga wakati akipokea tani 80 za mbegu katika kituo cha reli mkoani Tabora jana.
Alisema kwamba kutokana na mahitaji ya wakulima kanda hiyo imewalazimu kuanza kusambabza mbegu hizo mapema kwa ajili ya wakulima kuwahi mandalizi ya msimu wa kilimo.
Chiwanga aliendelea kusema kwamba Asa kwa kanda hizi mbili itasambaza mbegu hizo kwa njia ya Reli ili kupunguza Gharama za usafiri ,kwani usafiri wa Reli nirahisi sana tofauti na kukodi magari .
“Tani hizo 80 kama wangetumia usafiri wa malori yangetumika zaidi ya magari 8 ya tani kumi jambo ambalo Gharama zingeogezeka mara dufu”alisema Chiwanga
Hata hivyo alisema kwamba kwa upande wa wilaya na mikoa ambayo ipo kando ya barabara kuu ya kanda wataendelea kusafirisha kwa magari ambapo hada sasa wamesha sambaza tani 30 katika wilaya za Igunga ,Nzega na upande wa mikoa ya ziwa.
Mfanyabiasha wa Pembejeo wilaya ya Nzega Mkoani Tabora John Songo alisema kwamba ASA ni mara ya kwanza kusambaza mbegu kwa njia ya Reli jambo ambalo linaonesha wakala amedhamiri kuwasaidia wakulima wa mazao mbalimbali yanayosazalishwa na ASA.
Alisema hali hiyo itasaidia kupunguza bei za mbegu bora za kilimo zinazosambazwa na ASA katika mkoa wa Tabora.
Naye mfanyabiashara Yuda Mayila alipongeza wakala kwa kuanza kusafirisha pembejeo kwa njia ya Reli kitu ambacho kitasaidia sana kupunguza Gharama za kuwafikia walaji ambao ni wateja.
Hata hivyo Hakidum Mkuyu ambaye ni miliki wa duka la Pembejeo la Kachoma la mjini hapa alisema hilo ni jambo la kheri kwani walikuma mwaka huu watanufaika sana kwa bei ndogo za mbegu bora za mahaindi hasa Situka M .1 zinazosambazwa na wakala wa mbegu bora za kilimo nchini ASA.
Aliwataka wakala kuanza kusambaza mbegu bora za Alizeti kwani zimeandimika sana mkoani Tabora .
Alisema kwamba wananchi wanaziitaji mbegu hizo kwa wingi ili kukupambana na kasi ya uongezeko la bei la mafuta nchini.