Wazee mbalimbali wakiongoza maandamano katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika kimkoa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma Leo October 1,2021.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na Wazee pamoja na wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika kimkoa Wilayani hapo leo October 1,2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akizungumza na Wazee pamoja na wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ambayo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani hapo leo Oktoba 1,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat Maganga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani hapo leo Oktoba 1,2021.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk. Fatma Mganga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1,2021.
Mwenyekiti wa wazee Mkoa wa Dodoma mchungaji Petro Mpolo,akisoma risali kwa niaba ya wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1,2021.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh.Philip Mangula,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1,2021.
Baadhi ya Wazee Wilayani Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1, 2021
Baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Dodoma wakicheza muziki kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika kimkoa Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1, 2021.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akitoa zawadi kwa Wazee wa Wilaya ya Mpwapwa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Wazee ambayo Kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika Wilayani hapo leo Oktoba 1,2021
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akipokea zawadi kutoka kwa Wazee wa Mkoa wa Dodoma katika siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika kimkoa Wilayani Mpwapwa leo Oktoba 1, 2021.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,amewataka wadau wa Maendeleo kushirikiana na Serikali kuandaa mazingira rafiki kwa Wazee kukutana kuweka mipango mbalimbali ya Maendeleo.
Kauli hiyo aimetoa leo October 1,2021 wakati wa maadhimisho siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Mhe. Mwanaidi amesema kuwa Wazee wanakuwa wapweke kwa kukosa maeneo ya kuwakutanisha na kubadilishana mawazo na uzoefu katika mazingira mbalimbali wanayoishi.
Aidha ameeeleza kuwa miongoni mwa mambo ambayo Wazee wanatakiwa kupewa kipaumbele ni mawasiliano hasa wakati huu wa mabadiliko ya teknolojia.
“Makundi haya hayapati fursa ya kunufaika na teknolojia au mara nyingi hayanufaiki katika fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia. Hivyo, kama nchi tunao wajibu wa kuhakikisha wazee wanapata fursa sawa” amesema Mhe. Mwanaidi.
Amesema kuwa bajeti ya Afya imeongezeka ili kusaidia kuboresha huduma kwa wazee ikiwemo huduma za afya kutoka sh. bil 31 hadi bil. 270.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesisitiza jukumu la kuwatunza Wazee ni la familia na Jamii
Ametoa wito kwa Jamii kuwakemea wale ambao hawatunzi Wazee wao na ikitokea mzee hana mtu wa kumhudumia Serikali imeweka utaratibu wa kuweka makao na hivi sasa kuna makao 13 nchini.
“Tusipowatunza wazee ni dhambi kubwa, utakuta mzee ana watoto wengi lakini wanashindwa kumtunza pamoja na kuwa na uwezo huo. Serikali itatimiza wajibu wake lakini Jamii ina wajibu wa kwanza” amesisitiza Jingu.
Ameongeza pia mabaraza ya wazee ni fursa muhimu ya Wazee kukutana na kujadili masuala yao ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya upweke, hivyo yatumike vizuri.
Awali akisoma Mwenyekiti wa wazee Mkoa wa Dodoma mchungaji Petro Mpolo wameishukuru Serikali kwa kukamilisha zoezi la uundaji wa mabaraza ya wazee katika ngazi zote ambapo kilichobaki ni kuunda Baraza la Mkoa.
Aidha wameshukuru utaratibu uliowekwa na Waziri wa Afya wa kutoa huduma kwa Wazee kwa njia ya mtandao kila Jumamosi ambapo wanasikilizwa changamoto zao na kutafutiwa ufumbuzi.
Wazee hao walibainisha changamoto mbalimbali zinazotokana na uzee na kuomba Serikali iharakishe kuzifanyia kazi ikiwemo upatikanaji wa kadi za matibabu, upungufu wa dawa, kutoshirikishwa kwenye vikao vya maamuzi na kusumbuliwa na magonjwa kama tezi dume.
Aidha, wameiomba Serikali kusimamia utekelezaji wa maagizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Wazee kuelewa umuhimu wa kadi ya bima
Maadhimisho hayo ya siku ya Kimataifa ya Wazee hufanyika kila Oktoba Mosi, ambapo mwaka huu yamefanyika katika ngazi ya Mkoa yakibebwa na Kaulimbiu: “Matumizi Sahihi ya Dijitali kwa Rika zote,”