Picha na Tiganya Vincent
***********************************
NA TIGANYA VINCENT
Jumla ya Wazee 77,064 wametambuliwa na kuwapa vitambulisho vya msamaha wa malipo ya matibabu kufuatia maelekekezo ya Mwongozo wa Msamaha wa matibabu Mkoani Tabora
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya wazee Duniani chini ya ujumbe wa usemao “Matumizi sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa rika zote”
Alisema kati ya hao Wazee 24,051 wamepatiwa msamaha wa kulipia gharama za matibabu yenye thamani ya shilingi milioni 161.2 kutoka katika zahanati, vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri za Mkoa wa .
Balozi Dkt.Batilda alisema kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2020 hadi Juni 2021 imetoa misamaha ya matibabu bure yenye thamani ya shilingi milioni 40.9 kwa wazee 6,816.
Aidha Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali wazee kwa kuhakikisha huduma zote zinapatikana.
Balozi Dkt. Batilda alisema kwa kuthibitisha hilo tarehe 7 Mei 2021, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samia Hassan Suluhu alikutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kwa niaba ya wazee wote na kutoa maagizo ya kutatua changamoto zinazowakabili wazee.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Ofisi za wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wahakikishe wanatenga bajeti ya kutengeneza vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wasiokuwa na Bima ya Afya (NHF) au ICHF.
Ameongeza Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wahakikishe wanasimamia utoaji wa huduma bora kwenye madirisha ya wazee na kuendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa kwa wazee unakuwepo.