Katibu Mkuu Wizara ya Maji ,Mhandisi Anthony Sanga,akifungua Kikao kazi cha kujadili hatua ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu kilichofanyika jijini Dodoma
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Mkoani Simiyu wa Kampuni ya GITEC-IGIP ya Ujerumani,Christopher Batzlen,akitoa taarifa ya hatua ya utekelezaji wa mradi katika Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji ,Mhandisi Anthony Sanga,(hayupo pichani) wakati wa Kikao cha kujadili hatua ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu kilichofanyika jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Uendashaji na Matengenezo na Mabadiliko ya Tabianchi Mkoani Simiyu,Mhandisi Mwajuma Maziri akiwasilisha Mada katika Kikao kazi cha kujadili hatua ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu kilichofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maiji, Mhandisi Anthony Sanga amemtaka Mhandisi Mshauri kuzingatia uendelevu katika utekeleza wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Smiyu (Simiyu Climate Resilience Project).
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati wa katika kikao cha majadiliano kuhusu utekelezaji wa mradi killichohusisha wataalam wa Wizara ya Maji, uongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wote watakaohusika na utekelezaji wa mradi.
Mhandisi Sanga amesema mradi huo wa kimkakati ni miongoni mwa miradi mikubwa mitatu inayotekelezwa na Serikali katika sekta ya Maji utatekelezwa kwa gharama ya takribani sh. biloni 4a0 zitakazotoka kwa shinka la Green Climate Fund (GCH, Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (Kw) na Serikali ya Tanzania,
Amesema kuwa Mkataba huo unatarajiwa kusaini hivi karibuni ili kuendelea na utekelezaji rasmi wa mradi huo.
”Mradi huu wenye awamu mbili za utekelezaji, awamu ya kwanza ikianza na wilaya za Busega, tilima na Bariadi, awamu ya pill katika wilaya za Maswa na Meatu ni lazima Uzingatie mpango wa muda mrefu kutokana changamoto ya hali ya ukame katika mkoa wa Simiyu”
Mhandisi Sanga amesema kuwa utekelezaji wake kuhakikisha huduma ya uhakika kwa wananchi wote mkoani humo na nafasi ya kuongeza uwezo wa kuika maeneo mengi zaidi miaka jayo.
Amesema kuwa Kwa kuzingatia vigezo vya uendelevu wa mradi tumerudia usanifu wake na kuboresha baadhi ya vipengele vya kazi ikwemo kuongeza uwezo wa chanzo kutoka lita milioni 20 mpaka milioni 54.
Ameongeza kuwa uwezo wa miundombinu hususan matenki ya maji na uwezo wa kutosheleza mahitaji kwa wananchi mpaka mwaka 2035 kwa lengo la kupata matokeo makubwa zaidi. amesisitiza Mhandisi sanga.
Mradi huu wenye lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi mkoani Simiyu unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka 4 (Julai 2021-Agost 2025) na kunutaisha wakazi wapatao 495,000 kwenye maeneo ya usambazaji wa huduma ya majisafi na salama, usafi wa mazingira, kilimo cha umwagiliaji na mifugo, lengo likiwa ni kutatua changamoto mbalimbali zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.